Wednesday, July 30, 2014

Hizi Picha Za Patrick Bashizi Na Mkewe Maggie Seluwa Zina Tatizo !

Picha za msanii wa filamu na muziki Patrick Bashizi anayeishi Norway na kufanya kazi kwa ushirikiano na wasanii wenzake wa Scandinavia zimezua maswali kwa baadhi ya watu hasa wafuatilia habari na maisha ya mastaa ikiwemo baadhi ya mitandao kijamii na blogs. Picha hizo zinamuonyesha Bashizi akiwa na mkewe Maggie Seluwa akionyesha tumbo la ujauzito(baby bump).
Picha hizo niliziona kupitia akaunti ya Bashizi ya Facebook wakati alipoziweka siku ya kwanza na niliona ni kawaida tu kwasababu alichoonyesha Maggie ni tumbo pekee kitu ambacho kimekuwa kitu cha kawaida sana siku hizi sio kwa wasanii wakubwa tu wa marekani kama kina Ciara, Lil Kim, Shakira na wengineo ambao mara kibao tumeona wakionyesha baby bump.

 bali hata kwa wasanii kadhaa wa Afrika na Tanzania wamekuwa wakionyesha tumbo la ujauzito na wengine kupiga picha beach wakiwa kwenye swimsuit huku ujauzito ukiwa mkubwa. Au pengine ni kwasababu Maggie Seluwa licha ya kuigiza filamu pia ni msanii wa gospel ndiyo maana wengine wakajiuliza maswali !. Lakini siku hizi zinafanyika sherehe kibao huku Afrika hasa za watu maarufu na wenye pesa kwa mwanamke mjamzito anayetarajia kujifungua na sherehe hizo huitwa baby shower na tumbo la mjamzito hupigwa picha kwa baadhi yao. Lakini kwa ujumla kila mtu hufanya kitu fulani kwa maamuzi na matakwa yake binafsi na ukifikiria ni mume na mke wenyewe wameridhia nani wa kuwazuia !jibu ni hakuna maana kuna ule msemo unaosema mapenzi ni ya wawili.

Inasemekana haya yapo pia kwa baadhi ya makabili ya Afrika ingawa sina uhakika na hili. Je wewe una lipi la kusema?

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment