Saturday, November 8, 2014

Hii Ndiyo Barua Ya Sitti Mtemvu Ya Kujivua Taji La Miss Tanzania 2014.

Sitti
Hii ndiyo barua ya Sitti Mtemvu aliyoiandikia kamati ya Miss Tanzania kuhusu kujivua taji baada ya kuandamwa na skendo ya kudanganya umri. Taji hilo kwasasa litachukuliwa na Lilian Kamazima ambaye alishika nafasi ya pili, huku Jihani akishika nafasi ya tatu licha ya kupewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo.

"Baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu. Wameniwekea maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati siyo.

Shutuma hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu. Sasa kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014.

Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.

Leo nalivua rasmi taji nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo niliochukua."

                                                    Lilian Kamazima
                                                        Jihan Dimachk

No comments:

Post a Comment