Saturday, November 8, 2014

Mtasubiri Sana Mnaotaka Ndoa Yangu Na Gadner Dibibi Ivunjike: Jackline Pentezel


Star wa filamu Tanzania jackline Pentzel au Kauthar Dibibi kama anvyojulina sasa baada ya kufunga ndoa ya kiislamu amefunguka kuwa yeye na mumewe Bw. Gadner Dibibi bado wapo pamoja wanakula raha za ndoa yao inayokaribia miaka miwili sasa, Jackie amesema kuwa habari zinazovumishwa mtaani kuwa ameachika baada ya kugombana na mumewe si za kweli bali kuna watu wanaeneza hizo habari ili kutaka kuwachafulia ndoa yao lakini akadai watashindwa.

"nimekua napigiwa simu na watu tofauti na kuniuliza kua mmegombana na Dibibi kiasi ambacho Dibibi amehama nyumbani, hata mume wangu nae amekua akiulizwa hilo swali, tunabaki tunacheka tu, tunajua hao ni watu Wasiotutakia kheri lakini watashindwa tu sisi wala maisha yanasonga" alisema Jackie akizungumza na Swahiliworldplanet

No comments:

Post a Comment