Tuesday, April 15, 2014

Sina Haja Ya Kushirikishwa Kwenye Tuzo Za Action & Cut: Hemedy

Hemedy
Muigizaji wa filamu na mwanamuziki wa Bongofleva nchini Hemedy Suleiman amesema kuwa hana haja ya kushirikishwa kugombea katika tuzo za Action & Cut Viewer's Choice Awards 2014 ambazo zimeandaliwa na Bond Bin Sinan. Hemedy ameyasema hayo huku akiwa tayari amewekwa kwenye category ya Best Actor kupitia filamu ya Stella. "I really appriciate kwa wale waliohisi nafaa kuingia kwenye hizi tuzo hasa category ya best actor.........ila sioni sababu ya mashabiki wangu kupoteza muda na pesa za ku-vote kwangu!!!!........I'm not interested!!!.........tuzo yangu ipo kwa mashabiki always and am so proud of what I do!!!.....#pappination" ameandika star huyo kupitia Instagram.

Monday, April 14, 2014

Bazazi Na Chakubimbi: Filamu Ya Animation Toka Kwa Mtanzania Edwin Kileo.

Edwin Kileo ambaye ni mtaalamu wa subtitles katika filamu za Tanzania anakuja na kitu kipya kikali yaani filamu za animation na mastaa wa filamu Tanzania pia wataonekana katika kazi hizo za filamu za animation toka kwa Edwin ambaye kwasasa ameachia trailer ya Bazazi Na Chakubimbi inayoonekana hapo chini, Pia anatengeneza game na project zote hizo zitarushwa hewani katika Tv stations za Tanzania.

Photos: Red Carpet Looks From The 2014 MTV Movie Awards.

Winners Full List: MTV Movie Awards 2014.

The 2014 MTV Movie Awards were handed out Sunday at the Nokia Theatre in Los Angeles. Below are the winners of various categories.

Jackline Wolper Na Mtunisy Wasubiriwa Kwa Udi Na Uvumba

Mtunisy
Mastaa wa filamu nchini Tanzania Nice Mohamed "Mtunis" na Jackline Wolper wanasubiriwa kwa hamu kubwa na filamu yao mpya ya Tomboy(Jike Dume) ambapo Wolper amecheza kama jike dume huku Mtunisy akiwa kama kocha wa team ya michezo huku Wolper akicheza kama captain. Filamu hiyo ni kali sana kwa mujibu wa Mtunisy mwenyewe ambaye ni mmoja wa waigizaji wa kiume wanaodaiwa kuwa na mvuto mkubwa kiasi cha kuwapa wazimu kinadada wengi.

Filamu Ya Jicho Langu Toka Kwa Odama Yaendelea Kutikisa Sokoni.

Filamu ya JICHO LANGU toka kwa Odama bado inadaiwa kuendelea kukimbiza sokoni kama kawa. Filamu hiyo yenye kisa cha kusisimua yupo Odama, Salim Ahmed"Gabo" Thadeo Alexernda na Grace Mapunda. Hakikisha unanunua nakala yako halisi sasa.

Photos: Actress Faiza Ally on Vacation In Hong Kong.

Tanzanian Swahili movies actress Faiza Ally is enjoying her vacation in Hong Kong, Faiza is in a relationship with Bongofleva legendary Joseph Mbilinyi "Sugu" who is also Mbeya Mjini's member of Parliament. Faiza and Sugu have a daughter called Sasha. Look pics below

Kipindi Cha Action & Cut Chaingia Ubia Na Swahili Talk Radio Ya Nchini Denmark.

Bond
Kipindi kinachohusu masuala ya filamu cha Action & Cut kilicho chini ya Bond Bin Sinan ambaye ni mtangazaji, muigizaji, mtayarishaji na muongozaji wa filamu Tanzania kimeingia ubia na Swahili Talk Radio ya nchini Denmark ili kushirikiana na wasanii wanaofanya filamu za kiswahili katika nchi za Scandinavia na ulaya kwa ujumla ambao wanaonekana kupata inspiration kutoka filamu za Tanzania ambazo ndiyo kitovu cha filamu za kiswahili na lugha yenyewe ya kiswahili. Akizungumza na Swahiliworldplanet Bond alisema "now kipindi changu cha Action & Cut kimeingia partnership na kituo cha Swahili Talk Radio cha Denmark hivyo ni neema kwa wasanii wa Ulaya kufanya interviews moja kwa moja na zikarushwa katika kipindi changu , pia itakuwa ni neema kwa wasanii wa Scandinavia kujitangaza Afrika mashariki kwani wengi wao wanafanya filamu za Kiswahili pia jambo lingine ni wasanii wa hapa kuweza kufanya kazi au kushirikiana na wasanii wa Ulaya kupitia ushirikiano huu. wote kwa pamoja tuna malengo makubwa zaidi ya kuhakikisha filamu za Kiswahili zinafika mbali"

Filamu Ya "Sio Sawa" iliyowakutanisha King Majuto, Salehe Lufedha Na BabyLove Kuingia Sokoni Tarehe 24 April.

Filamu Kali ya SIO SAWA itaingia sokoni tarehe 24 Alhamis ijayo. Filamu hii imewakutanisha wasanii wakali kama vile King Majuto, Babylove Kalalaa, Salehe Lufedha na Modest Bafite. producer ni Salehe Lufedha huku muongozaji akiwa ni Felix Owino. Hakikisha unanunua nakala yako halisi ya filamu hii yenye kisa cha kusisimua ili ufaidike na kuburudika na familia yako.

Muhidini Gurumo Afariki Dunia

Mwanamuziki mkongwe wa dansi nchini Muhidini Gurumo amefariki dunia jana jumapili tarehe 13 April baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kujaa mapafu. Gurumo amefariki akiwa na umri wa miaka 74.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amen