Monday, December 24, 2012

KUFANANA KWA MAKAVA YA FILAMU KWATOKEA HOLLYWOOD NA BOLLYWOOD

Nimekutana na hili kava la muonekano wa kwanza(first look teaser poster) wa filamu mpya ya kihindi MURDER 3 inayotarajiwa kutoka mwezi wa pili tarehe 15 mwakani lakini limeonekana kufanana sana na la filamu ya hollywood iitwayo JENNIFER'S BODY iliyotoka 2009 na kuchezwa na Megan Fox na kuongozwa na Karyn Kussam, Filamu hii ya murder 3 imeongozwa na Vishesh Bhatt na kuchezwa na Randeep Hooda na hata story za hizi filamu ukiziangalia ni za kutisha kiasi flani lakini imekuwa vigumu kujua kama kuna aliyemuibia mwenzake wazo au mawazo yamegongana bila kujua ingawa story hazikaribiani kivile na murder sehemu ya 1 ilitoka mwaka 2004 , jennifer's body kutoka hollywood ilitoka mwaka 2009 ,murder 2 ilitoka 2011 na murder 3 itatoka february mwakani so ni vigumu kujua kama muonekano wa kwanza wa hili kava umeigwa kutoka hollywod au lah maana murder 1 ilitoka muda kuliko filamu hii ya hollywood.
Nimejaribu kuandika huu mgongano ili watanzania na watengeneza filamu wa kitanzania waone kuwa hata nje mawazo yanagongana siyo Tanzania pekee ambao wanatuhumiwa kuiga filamu za nje ila wakati mwingine siyo kuiga bali mgongano wa idea bila kujua, ila hili kava la filamu ya Bollywood ni muonekano wa kwanza wa promotion ya hiyo filamu hivyo yanaweza kutolewa mengine hasa film critics wakianza kazi yao lazima litabadilika BOLLYWOOD FILM
HOLLYWOOD FILM

No comments:

Post a Comment