Monday, December 24, 2012

EXCLUSIVE INTERVIEW WITH UPCOMING MODEL/ACTOR LOTA MOLLEL

wakati mwingine unapoangalia TV au hata kutembea barabarani unaweza kuona baadhi ya watu wakiwa wametokea kwenye matangazo katika mabango makubwa/billboards ila wengi wao wakiwa hawana mvuto katika hayo matangazo ya TV au billboards na makampuni makubwa nchini sielewi ni kwanini huwa hawatumii wanamitindo wenye vigezo kama LOTA MOLLEL ambao wamejaa nchini licha ya makampuni haya kudhamini fashion shows mbalimbali na kuwa karibu na madizaina ambao wangeweza kuwasaidia kupata wanamitindo wazuri kama Lota kwa ajili ya Matangazo ya bidhaa zao, mmoja wa wanamitindo wa kiume anayekuja kwa kasi sana na pia muigizaji mpya wa filamu za kiswahili. Ili kupata kumjua zaidi modo na muigizaji huyu anayependa kucheza filamu za kimapigano/action movies licha ya kushauriwa acheze filamu za kimahaba kutokana na mvuto aliyonao kwa wasichana wengi tulimuuliza machache just for you........!!!!!1
SWALI:Unaweza kutueleza machache kuhusu wewe, yaani umri wako, elimu na ni lini uliaza uanamitindo ?
LOTA:Well,.. Naitwa Lota Mollel nimezaliwa miaka 20 iliyopita ,kwa wakati huu mimi ni mwanafunzi wa multimedia na graphics, na kuhusu lini nilianza uanamitindo nafikiri ni mwaka huu baada ya kwenda kwenye shindano la kutafuta wanamitindo lililoandaliwa na Millen Magese kutokana na watu kuniambia nafaa kuwa modo,ingawa sikufanikiwa kushinda ila wengi walinipa moyo kuwa niendelee nitafanikiwa na ndiyo maana nimeanza kuona mwanga mbele yangu.
SWALI:Umetokea katika shows ngapi mwaka huu, na je ni mbunifu gani wa kitanzania unampenda ,mwanamitindo gani wa kitanzania anakuvutia na ni yupi mwanamitindo wa kimataita unakubali kazi zake?
LOTA:nimetokea kwenye shows karibia zote mwaka huu, swahili fashion week, maridadi fashion show, dar fashion festival,usiku wa khanga za kale na nyinginezo, mbunifu wa Tanzania ninayemkubali ni Martin Kadinda, kwa wanamitindo wa kitanzania namkubali Daxx Hans ananipa moyo , kimataifa namkubali Rob Evans na Tyson Beckford ningependa miaka michache ijayo nifikie mafanikio yao.
Swali: Hembu tueleze, una girlfriend au bado upo upo tu kwanza...., subiri kidogo!... una kipaji cha ziada zaidi ya uanamitindo?
LOTA:Bado nipo single mzee!..Ndiyo mimi ninacheza karate kama mchezo ninaoupenda na pia nimeanza kuigiza filamu na kutokea kwenye video kadhaa za wasanii wa bongofleva kama vile video ya my boo by Roseline na bum kubam ambayo ni video mpya ya Nick wa 2
SWALI: Wooh...!!!!kwa hiyo unaelekea kuwa muigizaji mashuhuri, ni filamu gani tayari umeigiza na je ni waigizaji gani wa kitanzania unawakubali kikazi?
LOTA:Nimeigiza filamu inaitwa exhibit ambayo nimeigiza kama bodigadi wa mzee magari, pia kuna filamu mpya inakuja ambayo nimepewa nafasi kubwa sana na nimeigiza na mastaa kama vile Elizabeth Chijuba maarufu kama Nikita,Mzee Magari, Kelvin, Bad boy na wengineo and in the film nimefanya action za kufa mtu kwa hiyo mashabiki wangu watarajie vitu vipya kutoka kwa Lota "The unstopable". Also kuna director amenifuata kwa ajili ya filamu yake mpya but things are not yet to be finalised for the film and my character.Namkubali Nikita na Bad boy ni waigizaji wazuri
SWALI:Umefaidika na nini mpaka sasa baada ya kuwa mwanamitindo na muigizaji, yaani baada ya kuanza kuwa maarufu umepata faida gani? na nini ungependa kuwaambia mashabiki wako kwa ajili ya ujio wako kwenye filamu ?
LOTA;Kiukweli bado sijaanza kupata faida ile ninayoitaka zaidi ya kujuana na watu wengi na kuwa rahisi kufanya baadhi ya issue zangu kwa hiyo bado naendelea kuvumilia nikitarajia mazuri zaidi huku nikiendelea kupigana zaidi. kuhusu mashsbiki wangu sina cha kuwaambia zaidi ya kuwaomba waendelee kunisapoti na kusubiri kazi zangu zinazokuja mwaka ujao hivyo nawatakia kheri ya x-mass na mwaka mpya. -photos by various sources-

No comments:

Post a Comment