Wednesday, July 30, 2014

Nimefilisika Sababu Ya Kuendekeza Sifa, Wanawake Na Matumizi Mabaya Ya Pesa: Mr.Nice

Mr.Nice na Diamond
Mr.Nice ambaye ni mmoja wa wasanii wakongwe wa muziki wa Bongofleva aliyetamba sana mwanzoni mwa miaka ya 2000 na nyimbo kibao zikiwemo Kikulacho, na Kidali Po amesema kuwa kufilisika kwake kiuchumi na hata kimuziki kumetokana na kupenda sifa zisizo na maana toka kwa wapambe, kuendekeza wanawake na matumizi mabaya ya pesa pasipo kuwasikiliza watu waliokuwa wakimshauri vizuri. Na baada ya kufilisika wale wote aliokuwa nao wakila maisha wamemkimbia. Akizungumza na Globalpublishers Mr,Nice alisema.......

"Enzi zangu nani asiyejua kuwa nilikuwa natembea na kundi la mabaunsa, mademu na kila kumbi nikiingia basi kila mtu atajua kama Nice yuko ndani lakini mwisho wa sifa zile ni nini? Si ndiyo zimenifikisha hapa nilipo, Nilikuwa na kila aina ya kamati ya ufundi, mashehe, wachungaji na maaskofu, wote walikuwa wangu, lakini kwa kuwa nilikuwa nataka sifa, dua zao zilikuwa kazi bure kwa sababu nilikuwa mtu wa starehe"

Mr.Nice ambaye pia amejaribu mara kadhaa kutaka kurudi kileleni kwenye muziki bila mafanikio ametoa ushauri kwa wasanii wengine akiwemo Diamond kwa kusema "Diamond kwa sasa anawika, anakubalika sana, ni kama ilivyokuwa kwangu. Namsihi asijisahau. Maisha yanabadilika. Namtakia mema ndiyo maana namshauri. Aachane na maisha ya kuwafurahisha watu, atengeneze maisha yake yajayo.
“Kuna wakati muziki unakataa, hapo ndipo mawekezo yake yatakapomfanya aendelee kuishi maisha bora bila muziki,
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment