Wednesday, July 30, 2014

Diamond: AFRIMMA Walitangaza Nimeshinda Tuzo 2, Sheddy Clever Pia Walimtangaza Kushinda.

Sintofahamu ilitokea baada ya tuzo za AFRIMMA awards kufanyika nchini Marekani juzi weekend na Diamond kudaiwa kutwaa tuzo mbili ya best male eeast Africa na best collabo My Number One ft Davido lakini katika mtandao wa tuzo hizo waliandika Diamond kushinda tuzo moja. Hta hivyo Diamond amewasili leo nchini na kutolea ufafanuzi wa suala hilo kwa kusema yeye alitangazwa kupata tzuo 2 na hata Shedy Clever producer wa My Number One alitangazwa kuwa mshindi lakini alishangaa baadaye tuzo nyingine alizotajwa kutokup.............

"Hata producer ambaye alikuwa ametangazwa ameshinda ni Sheddy Clever kwa sababu walimuonesha mpaka anapiga kinanda, maclip yake. Kama waliweza kuedit hata vinanda vyake anapiga yuko studio ina maanisha yeye ndiye alikuwa ameshinda.  Na wakatangaza collabo bora la kwangu mimi na Davido. Kwa sababu tuzo hii ndiyo tulienda kupewa kwenye stage kabisa pale. Lakini nyingine zilitangazwa kwenye TV.
“Lakini ghafla, mpaka kesho yake tukauliza mbona hatupewi tuzo zetu mpaka sasa hivi. Kwa sababu hata dada Jide naamini anaweza kupata leo au muda mfupi leo.  Sasa baadae wakaanza kusema kuna vitu vilikosewa sijui nini na nini…sikutaka tena kucomplain, kwa sababu nimeshapata yangu hii sikutaka kuleta matatizo mengine.” 

No comments:

Post a Comment