Tuesday, October 21, 2014

Timoth Conrad Atembelelea Ofisi Za Makao Makuu Ya Google Nchini Marekani.

Mtengeneza filamu na editor maarufu wa filamu nchini Tanzania Timoth Conrad ametembelea ofisi za makau makuu ya Google nchini Marekani aliko sasa ambapo alienda kuhudhuria tuzo za Silicon Valley African Film Festival 2014 ambapo filamu yake ya Dogo Masai ilinyakuwa tuzo katika kipengele cha Best Afrcan Feature Film kwa kuzimwaga filamu za S.Africa, Nigeria, Misri, Malawi na Uganda.

Tico ameweka picha na kuandika "Katika matembezi nimepita kwenye office kuu za GOOLE. Hiki ni moja kati ya vitu nilivyojionea. Hizi zote ni baiskeli za kampuni kwa kua office zao ninyingi ambazo zitakutaka kutembea umbali mrefu kutoka ofc moja kwenda nyingine wameweka baiskeli za bure unaitumia unaiacha popote. Hakuna kuondoka nayo. Nambie ingekua bongo zingekua zimebaki ngapi kwa mda wa wiki tuuu?"


No comments:

Post a Comment