Kutoka kushoto ni Rehema akiwa na Binti yake |
Rehema akiwa na mume wake |
SWP: Wewe ni mwenyeji wa wapi na ulianza utangazaji lini?
REHEMA: Mimi Mtu wa Tanga. nilizaliwa Ocean Road Hospital nimekulia Dar es salaam.
SWP: Uliondoka lini nchini Tanzania kwenda Denmark?
REHEMA: Mwaka 1993 niliondoka Tanzania kuelekea UK lakini 1996 nikahamia Denmark mpaka leo.
Rehema akiwa kwenye interview na star wa filamu Tanzania Lucy Komba |
REHEMA: Kwanza toka nikiwa mtoto nilikua namuweka juu sana baba yangu mdogo ambaye alikuwa mtangazaji wa Radio Tanzania Ayubu Mtawazo, alipokuwa anakuja kututembelea nyumbani nilikua nataka aongee kama yuko kwenye radio , hio ilikua inspiration inspiration ya kwanza.
Pili mume wangu ni mtangazaji wa Radio 1 ni Radio station hapa Denmark Jina lake ni Søren Rasmusen, ajulikanae kama NewsSøren kutokana na kazi yake kama msomaji wa taarifa za habari pia , anatangaza kipindi cha asubuhi ambacho ni matokeo ya kila siku.
Tatu, baada ya kuishi ulaya kwa zaidi ya miaka 20, niliona kuwa tunapaswa tutafute mahali ambapo tunaweza kuwa free na kujiweka wazi kwa lugha yetu, kwa usaidizi na mume wangu jibu langu likawa Swahili Talk Radio.
Dj wa kipindi cha hakuna kulala toka Swahili Talk Radio |
REHEMA: Kitu ninachokifurahia katika kazi yangu ya Utangazaji ni kuweza kuzifikia jamii za kiafrika kwa kiasi kikubwa na kwa wakati mmoja, kitu ambacho hatukuwa na uwezo nacho miaka miwili iliyopita, naamini kwamba mawasiliano ni muhimu sana kwa jamii.
SWP: Changamoto unazokumbana nazo kama mtangazaji wa kiswahili Ulaya ni zipi?
REHEMA: Ni ngumu kwa waafrika kuingia kwenye soko la wazungu... ningepeda sana radio yangu iwashawishi wazungu kuwapa waafrika nafasi na sio tu wasanii bali waafrika wote wenye vipaji, mimi napigania nafasi yetu bara la Ulaya, najua ni ngumu lakini i will make it.
SWP: Ni changamoto gani unazokumbana nazo toka kwa wasanii wa kiswahili wa huko ambao wengi sio watanzania na kiswahili chao huwa tofauti na Tanzania?
Rehema akiwa kwenye interview na Mr.Nice |
REHEMA: Kuhusu wasanii ambao sio watanzania kwangu mimi sina tatizo lolote kwanza mimi ni mkalimani professional nina Kampuni yangu African Work House ambayo mimi ndio C.E.O wa Kampuni hiyo, nafanya kazi na serekali kupokea wakimbizi na kuwa mkalimani katikati ya serekali na wakimbizi hao, na sio watanzania kwahiyo nimezoea najua kugeuza kiswahili changu inategemea naongea na mswahili wa wapi.
SWP: Je una watoto na wanajua kuzungumza kiswahili pia maana umekaa ulaya zaidi ya miaka 20 sasa
REHEMA: Nimebahatika kuzaa mtoto mmoja wa kike ana miaka 15.kuhusu kiswahili anajitahidi lakini hayuko mia kwa mia, najitahidi kumsaidia ili awe mia kwa mia. lakini mila na heshima za nyumbani zote nimemfundisha. sio mtoto tu na mume wangu ambaye ni Mdenish pia anajua mila zetu, na kiswahili kidogo.
SWP: Lini utamleta Tanzania huyo mtoto?
REHEMA: Kabla hajaenda chuo kikuu anataka kujakukaa kidogo Tanzania.
SWP: Swahili Talk Radio imeingia ubia na kipindi cha Action & Cut kilicho chini ya Bond ambaye ni mtangazaji wa mambo ya filamu je unaweza kutueleza zaidi hasa faida kwa wasanii wote wa huko na huku Tanzania?
REHEMA: Kuhusu mkataba wetu na Action & Cut ambocho ni kipindi cha Bond. baada ya mimi na Søren kum-study Bond na kazi zake tuliona ni mtu muhimu sana katika maswala ya sanaa kwa ujumla. Bond ni kijana ambaye ana upeo wa kufikiria upesi na kuona mbali yaani hard working boy. Na sisi kama African Work House ni sifa muhimu alizo nazo. ndio maana tumeingia nae ubia na mpaka sasa tulicho kitangaza ni kitu kidogo tu. tuko na vitu vingi viko mbele yetu kuhusu kazi zetu, miaka mitano ijayo mimi na Familia yangu tunataka kuja kujaribu maisha Tanzania,
Sasa hivi na Bond tunajaribu kuweka kuzifanya Swahili Movies za Ulaya kupata catagoties, nafasi kwenye Film Awards za Tanzania, ili na wasanii wa Kiswahili wa Ulaya wapate recognition
Watoto pia hupewa nafasi katika Swahili Talk Radio |
REHEMA: No no no Swahili Talk Radio is here to stay, Swahili Talk Radio nia kubwa ni kuweka Connection ya waswahili wa Afrika na bara la Ulaya yaani kwa wale wa ulaya kuwa wazi na kuongelea kinachoendelea ulaya na wa afrika wanaoishi Africa pia kupata nafasi kujua haswa Ulaya na mahali gani Wasije wakadhani ni peponi hapa. Swahili Talk Radio itasaidia watu kuwa wazi, kwenye radio na kwenye live Talk Show zetu.. maana haswa ya jina Swahili Talk Radio sio radio yakupiga tu muziki japo sasa hivi hatuna full time watu kwenye studio lakini itafikia hapo, hatutaki kuongea tu kwa kuongea. na idea zetu tunazi fanyia uchuguzi kabla hatujaziongelea.
SWP: Una lolote ambalo ungependa kulizungumzia ambalo sijakuuliza?
REHEMA: Kitu ambacho saa nyingine huwa kinanisikitisha kuhusu jamii za kiafrika huku ulaya ni kuwa ningependa kuwakumbushia kuhusu Elimu. Hapa elimu ni bure na unapewa pesa kwenda shule japo sio mamilioni. kwanini watu wengi hawatumii nafasi hii? Wakati wako watu Africa wanataka kusoma na hawana nafasi hii ! mimi naona sio fair.
Kwa upande mwingine pia tuko na reporter wetu nchini Canada anaitwa Llouise Mat yeye anaongelea sana mambo ya siasa.
Kwa kumalizia ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Abou wa Twaleb Entertaiment kwa kujitolea kutengeneza promo ya kipindi chetu kila Ijumaa.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
No comments:
Post a Comment