Saturday, April 19, 2014

Behind The Scenes: Faiza Ally Apata Deal La Kuigiza Filamu Ya Action Hong Kong.

Faiza Ally akifanya vitu vyake katika filamu hiyo
Star wa filamu nchini Faiza Ally ambaye pia ni mzazi mwenzake Mh. Joseph Mblinyi "Sugu" aliye mmoja wa waasisi wa muziki wa kizazi kipya amepata deal la kucheza filamu mpya nchini Hong Kong kitu ambacho hakukitarajia. Katika Filamu hii Faiza aliyejipatia jina baada ya kuigiza na Dr.Cheni character yake sio kubwa sana huku akionekana katika scene ya action akiwa ameshikilia bastola mbili mkononi.

 Alipoulizwa na Swahiliworldplanet kuhusiana na project hiyo Faiza ambaye aliwahi kuingia kwenye mbio za Miss Tanzania 2005 " Director wa filamu hii anaitwa Oliver, nimecheza scene fupi nikiwa kama mwanamke anayeibiwa na nimeingizwa kwenye hivyo movie na rafiki yangu ambaye ni mchina anaitwa Andwer yeye ni Kama katili katika filamu hiyo.. Jina bado halijatoka na stori inamuhusu msichana wa kichina ! Sijauliza mengi kwa sababu nimekuta kazi inaendelea hakukua na muda watu maongezi zaidi"

Kuhusu malipo kutokana na character yake katika movie hiyo Faiza alisema " Malipo ni mazuri sio mabaya kutokana na ukubwa wa kazi ni poa"

Alimalizia kwa kusema kuwa kuna project kubwa inakuja mwezi wa nane mwaka huu " kuna project kubwa inakuja mwezi wa nane Insha Allah tuombe Mungu mambo yasibadilike"

Faiza Ally alienda Hong Kong hivi juzi kati kwa mapunziko na kupata bahati hiyo ambayo inazidi kumuongezea uwezo na ujuzi kama mcheza filamu. Angalia zaidi picha za behind the scenes/utengenezaji wa filamu hiyo hapo chini
  

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni tarehe 24 April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment