Wednesday, July 16, 2014

VJ Penny Na Wema Sepetu Wamaliza Beef Lao Lililotokana Na Penzi La Diamond PLatnumz.

Wema Sepetu na VJ Penny wamemaliza beef lao lililokuwepo kwa muda mrefu sasa baada ya Penny kuingilia uhusiano wa Wema na Diamond. Hata hivyo Wema ameamua kumsamehe Penny wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
"Kwa moyo mweupe, nasema nimemsamehe Penny, hata nikikutana naye popote nitasalimiana naye kama kawaida. Nimeamua kuachana na yote, mimi ni binti wa Kiislam na nahitaji sana swaumu yangu ipokelewe vyema kwa Mungu." alisema Wema wakati akizungumza na GPL

Nae Penny alipotafutwa alisema "Siwezi kusema nitamchukia Wema ila nimekubali matokeo, sina tatizo naye tena ingawa najua hatuwezi kuwa marafiki tena  kama zamani, lakini yaliyopita yameshapita.”

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Filamu kali ya MUME BORA itaingia sokoni tarehe 30 July, usikose kununua nakala yako halisi.


Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment