Saturday, April 19, 2014

Action & Cut Awards Wakaa Chini Na Kundi La Bongo Movie Unity Kuweka Mambo Sawa.

Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity Steve Nyere na Bond
Mgongano uliokuwepo kati ya Kundi la Bongo Movie Unity katika tasnia ya filamu nchini na muandaaji wa tuzo za Action & Cut Viewer's Choice Awards Bond Bin Sinan umefikia ukingoni baada ya kukaa pamoja na kuyamaliza. Kundi hilo la Bongo movie lilikuwa na mashaka na mchakato uliotumika kuwapata nominees wa tuzo hizo na unakoelekea katika kuwapata washindi. Baadhi ya wasanii wa kundi hilo walitishia kujitoa ambapo wengi ndiyo niminees kuliko wasio wanachama wa kundi hilo.

 Akizungumza na Swahiliworldplanet mwandaaji wa tuzo hizo Bond Bin Sinan ambaye pia ni mtangazaji wa Action & Cut, muigizaji wa filamu alisema "Bongo Movie Unity walikuwa hawajaelewa mchakato ulianza vipi na unakwenda kuisha vipi na mpaka wengine walitishia kutaka kujitoa, nafurahi wameonyesha ushirikiano na mapenzi ya dhati kutuita kamati ya tuzo hizi za ACVCA, wametuuliza mambo mengi na tumewajibu kiufasaha, mwisho wametupa baraka zote na ukizingatia asilimia kubwa ya washiriki wanatokea katika unity hiyo hivyo nina imani mabo yatakwenda vizuri na mwisho tutafikia malengo tuliyojiwekea na tuzo zitakuwa za kihistoria Mungu akituweka hai"

                                                              Cloud na Bond
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni tarehe 24 April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment