Saturday, April 19, 2014

Lulu Aangua Kilio Baada Ya Kumwagiwa Pombe Mwili Mzima Na Kulowa Chapachapa.

Lulu akimwagiwa pombe
Screen diva wa filamu Swahiliwood Elizabeth Michael "Lulu" anadaiwa kumwaga chozi la kufa mtu juzi tarehe 16 wakati wa birthday yake iliyofanyika katika hoteli ya Regency, Mikocheni jijini Dar es salaam. Birthday hiyo iliandaliwa na marafiki wa karibu wa Lulu ambao sio mastaa na ilikuwa siri kubwa ili mapaparazi wasijue na kupiga picha kitu ambacho kilipelekea hata mastaa wenzake wasiwepo kwani hawakujua kwakuwa iliandaliwa na rafiki zake wasio mastaa

 Mida ya usiku mwingi Lulu alianza kumwagiwa pombe kuanzia kichwani mpaka miguuni na rafiki zake hao kiasi cha kulowa chapachapa kitu ambacho hakuwa amekitarajia kama ilivyo kwa birthday nyingi zilivyo na surprise na vituko kibao. Baada ya kumwagiwa pome mwili mzima star huyo mkubwa alianza kumwaga chozi la ukweli na kubadiliasha nguo. "Naamini alibadili hata nguo za ndani, maana alilowa pombe mwili mzima" kilisema chanzo kilichohudhuria party hiyo kikizungumza na GPL.
moja ya keke alizoandaliwa Lulu
Katika Birthday hiyo Lulu aliandaliwa keki tano na rafiki zake hao huku star aliyehudhuria issue hiyo ya kushtukiza akiwa Dr.Cheni peke yake. Lulu alizaliwa tarehe 16 April 1995 hivyo ametimiza miaka 19.

                                                                        Lulu
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni tarehe 24 April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment