Wednesday, October 29, 2014

TBC1 Yashika Mkia Kutazamwa Na Watu Kwa Mujibu Wa Utafiti Mpya, Ubaguzi Wa Kisiasa Watajwa.

Kwa hali ya kushangaza, kituo cha television cha matangazo cha TBC 1 kati ya vituo vinne maarufu vya matangazo ya habari nchini Tanzania kimeshika nafasi ya mwisho baada ya kufanyiwa utafiti,
Kwa habari za uhakika ni kwamba kituo kilichoongoza kuangaliwa na watazamaji wengi ni ITV kikifuatiwa na Star TV, nafasi ya tatu imeshikwa na Channel 10 na hatimaye TBC1.

Kwa utafiti uliofanywa na na TCRA imebainika kuwa ni aibu kama kituo television ambacho ni cha Taifa na ni UMMA kushika mkia nyuma ya vituo binafsi jambo ambalo ni hatari.

Vyanzo vya kuaminika vinadai kuwa TBC1 imefikia hapo baada ya kugundulika inabagua baadhi ya habari ya vyama vya siasa na kutoa habari ya chama kimoja tuu jambo ambalo siyo sahihi katika utashi wa utangazaji na kutofuata uhuru wa kiutangazaji ndani ya uongozi wa shirika la habari la Tanzania, 

Utafiti umeonyesha kuwa ili chombo cha habari kiweze kuangaliwa na watu wote wa vyama vyote ni lazima chombo cha habari kitoe habari bila kubagua vyama vya siasa maana watazamaji wana misimamo tofauti na itikadi tofauti, na kama chombo cha habari kikiamua kutoa habari kwa chama kimoja cha siasa basi ujue hapo watakaoangalia hizo taarifa za habari ni hao hao wa chama kimoja.

Watafiti pia walienda mbali zaidi na kukinyoshea vidole kituo cha taifa cha utangazaji kuwa ni chombo cha UMMA na kisipende kubagua baadhi ya taarifa za habari za vyama vya siasa kwa misingi ya kuelekezwa na wanasiasa au viongozi wa nchi maana madhara yake ni wananchi kushindwa kuangalia hicho kituo.

Mwisho wake kitashindwa kufanya biashara na hatimaye kutegemea tuu ruzuku serikalini na hapo ndo nchi itazidi kupata hasara badala ya kukiacha chombo kijiendeshe kwa uhuru. Wametoa mfano kama shirika la habari la Uingereza BBC lingefanya kama TBC inavyofanya basi nayo ingeishia kutazamwa tuu nchini uingereza na tena kwa watu wachache tofauti na ilivyo sasa BBC inatazamwa duniani kote.

Utafiti umeonyesha kuwa hivi vyombo vingine vya habari ITV, Star TV na Channel 10 vimepata watazamaji wengi kwa kuwa havibagui matangazo ya kada tofauti ya vyama vya siasa na hapo ndoo inasababisha waweze kupata watazamaji wa kutosha.

No comments:

Post a Comment