Flora Mvungi |
Akizungumza na Global Publishers star huyo aliyekuwa Miss Bagamoyo, Miss Pwani na Miss Kanda Ya Mashariki 2008 na baadaye kushiriki Miss Tanzania alisema kuwa wakati alipokuwa akiigiza igizo la Bongo Dar es salaam chini ya Dude Kulwa Kikumba alikuwa halipwi sababu alikuwa bado ni msanii mchanga kwa hiyo alikuwa bado anapigania kukuza jina lake na kuishia kuuza sura tu licha ya igizo hilo kukubalika kwa wengi. Akizungumza na Globalpublishers mazungumzo yao yalikuwa kama ifuatavyo............
Mwandishi: Je ulikuwa ukilipwa shilingi ngapi?
Flora: Kwa kipindi hicho kwa sababu nilikuwa nataka nijulikane nilikuwa silipwi chochote nilikuwa nauza jina na sura tu wala sikuwa naona shida yoyote.

Mwandishi: Siku ya kwanza kuonekana kwenye TV ulijisikiaje?
Flora: Ukweli nilikuwa na raha sana kila mtu mtaani kwetu na ndugu zangu walijua kwani niliwapa taarifa kwamba waangalie TV.

Mwandishi: Baada ya Bongo Dar es Salaam ulifanya kitu gani?
Flora: Nilikuwa napenda sana mpira wa miguu sasa siku moja nikiwa Uwanja wa Taifa nikiangalia mechi, mdau wa soka, Frederick Mwakalebela akaniambia anataka kuanzisha kampuni ya filamu lakini hajui aanzie wapi ndipo nikamuunganisha na Dude.
Baada ya kumuunganisha ndipo tukacheza filamu ya Septemba Eleven ambayo ndiyo filamu ya kwanza kucheza chini ya kampuni hiyo nikiwa muhusika mkuu.
Mwandishi: Nini kiliendelea baada ya hapo?
Flora: Kutokana na kucheza filamu hiyo nilijuana na mastaa wengi ambapo Wolper aliniunganisha na Lamata (Leah Richard) ambaye alikuwa akifanya kazi na Kampuni ya Daniel Basila (aliyekuwa mume wa Bahati Bukuku) nikacheza filamu iliyojulikana kwa jina la Passion.

No comments:
Post a Comment