Wimbo mpya wa mwanamuziki maarufu wa Tanzania AY ambao amemshirikisha Sean Kingston raia wa Jamaica-Marekani unaoitwa "Touch Me TouchMe" unatarajiwa kutoka November mwaka huu.
Akizungumza na Bongo5 AY amesema kuwa yeye na Sean Kingston wana ukaribu sana wa kikazi na pia kama marafiki kwasababu Sean Kingston ameaonyesha kumkubali AY na kusaidiana nae katika mambo mengi. Vilevile AY alisema kuwa hata mama yake Seam Kingstone anamkubali sana na kumchukulia kama mwanae na mara kwa mara hutoa comments kwenye instagram yake.
"Yaani huyu jamaa ananipa saupport asilimia 100% huwezi kuamini ni mtu ambaye si yeye tu hata mama yake mwenyewe tunawasiliana kwa hiyo ni family yaani, mama yake ananichukulia kama mtoto wake hata kwenye instagram yake ana-comment, halafu hii yote ni family ambayo nikienda Los Angels ndo watu wangu ambao ndo na-hamg nao"
AY pia alisema kuwa Sean Kingston hupokea dollar za kimarekani $30,000 ili kufanya collabo na msanii mwingine lakini kwa yeye AY imekuwa tofauti wamefanya bure kutokana na Sean Kingston kukubali uwezo na kipaji cha AY.
No comments:
Post a Comment