Monday, October 20, 2014

Sabby Angel Na Bob Junior Waangukia Katika Dimbwi La Mahaba Mazito.

Sabby Angel
Mahaba niue !....Gossip mpya ni kuwa actress anayekuja juu kwa kasi kama moto wa kifuu  Sabby Angel ambaye pia ni mwanamuziki wa kizazi kipya tayari anadaiwa kuwa kwenye dimbwi zito la mahaba na Bob Junior ambaye pia ni star wa Bongofleva na mmiliki wa Sharobaro Records.
Kwa mujibu wa chanzo makini toka kwa wawili hao kikizungumza na Swahiliworldplanet  jioni hii kimesema kuwa Sabby na Bob Junior wanapendana na mahaba yao yalianzia studio ya Bob Junior hivi juzi kati Sabby alipoenda kwa ajili ya issue zake za muziki ndio kila mmoja akamzimikia mwenzake.

Ukiachilia mbali hayo Bob Junior amekuwa akirusha comments na kuchat kimahaba na Sabby Angel kwenye mitandao ya kijamii hususani Instagram kama inavyoonekana hapo chini.

Hapo Sabby aliweka picha ya Bob Junior na Bob Junior kuanza kuchombeza

Bob Junior hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya wakati Sabby kwasasa anatamba sokoni na filamu ya Siri Ya Giningi huku filamu yake mpya ya Moto Wa Radi ikitarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu kuanzia sasa.

No comments:

Post a Comment