Monday, October 20, 2014

Kilichomtokea Aisha Bui Champata Batuli Pia, Batuli Afunguka Kwa Masikitiko.

Batuli
Habari mpya magazetini leo ni kuhusu muigizaji wa filamu nchini Aisha Bui kufanya vurugu ofisi za YUNEDA ambayo ni kampuni ya usambazaji wa filamu nchini kwa mdai ya kutomlipa aisha Bui
pesa yake kwa wakati na kumlipa nusu licha ya Aisha kusubiri kwa muda mrefu bila mafanikio huku mhusika akidaiwa kum-block Bui katika simu yake ndipo hasira zikampanda Aisha na kufunga kibwebwe mpaka ofisi hizo zilizopo Mbagala na kukinukisha. Batuli Yobnesh Yusuph nae amefunguka baada ya sakata hilo na kusema hata yeye yameshamtokea hayo kutokana na baadhi ya wasambazaji wasivyo waaminifu kutaka kuwadhulumu wasanii. Batuli ameandika.........

"Haya ndio tunayokutana nayo wasanii wa kike, Kiukweli kabisa wapo watu wanaoturudisha nyuma kila kukicha, Mbaya zaidi wanaofanya hivi ni wale wanaoheshimika kwenye jamii na sio kwamba hana uwezo wa kukulipa bali hufanya hivi kukukomoa tu, Binafsi nina maumivu kama ya @aishabuithebootybaby unafanya kazi na mtu kwa makubaliano fulani tena kwenye mazingira magumu matokeo yake mwisho wa siku anakudhulumu haji yako, Ukitupia picha mitandaoni unakutana na maswali kutoka kwa mashabiki "Tumekumic Hatukuoni Kwenye Movie Siku Hizi" Mazingira ya Ubabe, Dhulma, ndivyo vinavyotawala kwenye fani hii, Haipendezi na sio vyema kwa wale wenye tabia kama hizi, Acheni dhulma kwenye kazi, Mkumbuke tunaaga kwenye familia zetu kuwa tunakwenda kazini, Matokeo yake ukirudi nyumbani watu wanakushangaa badala ya kuhudumia familia wewe ndio unakuwa Matonya. Kesho na kesho kutwa unaandikwa magazetini unagombeae bwana watu wanakuona muhuni sasa kwa style hii ya kudhulumiana unategema mtu ajikimboe kwa njia gani?"

No comments:

Post a Comment