Monday, October 20, 2014

Kimenuka ! Sitti Mtemvu Kuvuliwa Taji La Miss Tanzania 2014, Jihan Kwenda Miss World 2015 !

Sitti Mtemvu
Baada ya watanzania na wadau wengi wa urembo na mitindo nchini kukinukisha kwa kuukataa ushindi wa Sitti Mtemvu kuvikwa taji la Miss Tanzania 2014 kwa madai hakuwa na sifa na ana umri mkubwa sasa kimenuka !...
Habari ambazo zimeandikwa leo mpaka magazetini ni kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Sitti kuvuliwa taji la Miss Tanzania 2014 huku issue ya umri wake ikiwa moja ya point kuu za kumvua taji hilo. Inadaiwa pia kuwa kwasasa wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania wamegawanyika ambapo kuna wasioukubali ushindi wa Sitti huku wengine wakiona sawa tu.

Habari zaidi zinadai kuwa kamati na waandaaji wa Miss Tanzania wanataka kumvua Sitti taji ili kuendelea kuweka taswira, imani na usafi wa shindano hilo kwa kuondoa kashfa ya upendeleo na rushwa kama ilivyo midomoni mwa watu kuhusu shindano hilo kwasasa baada ya Sitti kukataliwa kuwa Miss Tanzania 2014. Pia inadaiwa kuwa kamati ya Miss Tanzania ina hofu na issue ya Sitti kufika kwa waandaaji wa Miss World na hivyo kuweza kulizuia shindano la Miss Tanzania miaka kadhaa au kufuta ushiriki wao kabisa.

Inadaiwa zaidi kuwa ikiwa Sitti atavuliwa taji basi kuna uwezekano mkubwa Jihan Dimachk akaiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss World 2015 kutokana na watanzania wengi kumkubali na kudai ameonewa kuliko hata mshindi wa pili Lilian Kamazima.

Vigezo vinavyolalamikiwa kumpa ushindi Sitti ni utata wa umri wake huku wazazi wake mama akisema mwanae ana miaka 29 wakati baba mzazi na Sitti mwenyewe wakisema ana mika 18 huku passport yake ikionyesha ana miaka 25, umbo lake anadaiwa kuwa mnene hivyo kukosa sifa za umiss, anadaiwa kuwa na mtoto wa miaka 6-8, swali hakujibu vizuri huku akichanganya na lugha ya kifaransa ambayo awali hakuichagua, inadaiwa kuwa sifa zake hazikumzidi Jihan na Lilian Kmazima walioshika nafasi za pili na tatu.

Jihan

Jihan Dimachk ambaye watanzania na mashabiki wengi wa urembo wamelalamikia kuwa ameonewa yaani yeye ndiye alistahili kupewa taji la Miss Tanzania 2014.

No comments:

Post a Comment