Monday, October 20, 2014

Photos: Kweli Ommy Dimpoz Na Vanessa Mdee Wametoka Mbali, Soma Ujumbe Mzito Wa Dimpoz.

Dimpoz na Vanessa Mdee miaka michache nyuma kabla hawajawa maarufu kama ilivyo sasa
Kweli watu wanatoka mbali kabla ya kupata mafanikio ! wiki iliyopita picha ya Ommy Dimpoz akiwa anadandia treni miaka kadhaa nyuma pengine kuja Dar ilisambaa mitandaoni kama moto wa kifuu kwa watu kutoamini kuwa ndiyo Dimpoz wa leo huku wengine wakimtukana na kuandika yao wayajuao.
Msanii huyo mkubwa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwasasa ame-share picha nyingine akiwa na Vanessa Mdee kuonyesha kuwa wametoka mbali na hawajakutana upenuni kama baadhi ya watu wanavyofikiri. Ommy na Vanessa ndio wanaonekana katika hii picha Vanessa akimpokea Ommy ambapo leo hii tayari ni mwanamuziki maarufu nchini na wenye mafanikio ndani ya miaka michache. Kupitia Instagram Dmpoz aliweka picha hiyo na kuandika ujumbe huo hapo chini wenye funzo............

Picha ya Ommy Dimpoz iliyosambaa wiki ilopita na alivyo sasa


"Wiki iliyopita nimejifunza mambo mengi sana baada ya ile picha niliyodandia treni kusambaa kwenye mitandao kuna watu waliongelea km utani,kuna watu walinikebehi,wengine waliweka kwenye mitandao na kunitusi kabisa. ila nilichogundua Sio kila tunachokiona kwenye mitandao kina ukweli tujaribu kuwa wachunguzi,tuache mambo ya kucopy na kupaste jambo la mwisho kabisa siri ya Maisha anaijua mungu usimdharau mtu kwa muonekano unayemuona mshamba eti amekukuta mjini kesho ndo huyo huyo atakayekupa ajira tupendane tusidharauliane......Asante@vanessamdee kwa kupokea na fuko langu "

                                                                   walivyo sasa
😅😅

No comments:

Post a Comment