Saturday, October 18, 2014

Mashabiki Ethiopia Wamvamia Timoth Conrad Wakidhani Ni Ommy Dimpoz !

Tico
Wabongo waishio nchini Ethiopia wamemvamia msanii wa filamu nchini Timoth Conrad wakati akiwa Adis Ababa kuelekea Marekani wakidhani ni star wa Bongofleva nchini Ommy Dimpoz.
Akizungumza na Swahiliworldplanet tokea nchini Marekani Timoth ambeye yupo nchini humo kuhudhuria tuzo za Silicon Valley African Film Festival 2014 ambapo filamu yake ya Dogo Masai imependekezwa kuwania tuzo ya Best African Feature film alisema.....
Tico

"Nilipofika Adis Ababa(Ethiopia) nikavamiwa na wabongo na kuanza kunishangilia wakidhani ni Ommy Dimpoz. Ilikua balaa ikabidi nikubali kuwa ndio mimi poz kwa poz maana ningekataa wangeweza kunipiga mawe au ningemharibia soko omy nikafurahi nao... Sasa ililofika wakati wakuwapa namba ya simu na kutaja jina ilikua balaa. Nikamtajia mmoja kuwa asevu Timamu wakagoma wakaambizana andika jina wanalolijua wote wakaandika pos kwa pos(jina ambalo hutumiwa na Dimpoz) dah nikawa mpole. Eti jamani mimi nimefanana nae au yeye kafanana na mimi?" Alisema Tico huku akiwauliza watu mumpe jibu kama anafanana na Dimpoz au lah

                                                                  Ommy Dimpoz

No comments:

Post a Comment