Monday, October 13, 2014

Aunty Ezekiel Aitikisa Ndoa Ya Mh. Lazaro Nyalandu Na Faraja Kota ! Nyalandu Afunguka.

Aunty Ezekiel
Juzi gazeti moja la habari za mastaa nchini liliandika kuwa ndoa ya Mh. Lazaro Nyalandu ambaye ni mbunge na waziri wa maliasili na utalii nchini na Faraja Kota ambaye ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 2004 inatikisika kisa kikidaiwa ni star wa filamu nchini Aunty Ezekiel
kudaiwa kutoka na mh. Nyalandu mara baada ya kukutana nchini Marekani katikati ya mwezi September mwaka huu.

Aunty Ezekiel hakuzungumzia suala hilo mpaka sasa, hata hivyo Nyalandu amezungumzia suala hilo mbele ya waandishi wa habari baada ya magazeti kuandika habari ya yeye kudaiwa kuwa wapenzi na Aunty ikidaiwa ni ufujaji wa pesa za walipa kodi kwa alichokifanya kwenda kutanua na Aunty nchini Marekani. kwa mujibu wa Mtanzania Nyalandu akijibu madai hayo kwa kusema hakutanua na Aunty na wala sio wapenzi bali alienda Marekani alipoalikwa kama mgeni rasmi wa tamasha la Utamaduni na Utalii kupitia soko la wasanii wa Tanzania ikiwamo kuwatangaza wasanii kimataifa, alisema tamasha hilo liliendeshwa na blog ya Vijimambo 13 September mwaka huu.

Mh. Nyalandu kushoto na Aunty Ezekiel kulia walipokuwa Marekani
Alisema Aunty aliongozana na msaniii wa Bongo Fleva Cassim Mganga na safari yao iliratibiwa na waandaaji hao kwa ushirikiano na ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na sio yeye aliyempeleka Aunty nchini humo bali alisema wabaya wake kisiasa wakiwemo baadhi ya watendaji wa wizara yake na baadhi ya viongozi wa serikali ndiyo humchafua kwenye media kutokana na kutopenda utendaji wake kazi mzuri wa kutotaka kushrikiana na majangili.

"mimi na Aunty tulionana siku moja tu tena usiku wa tukio ambalo lilifanyika 13 September 2014 kwenye kilele cha sherehe ya utalii na baada ya hapo sikuwahi kuonana naye tena" Alisema Nyalandu

Na kuongeza "baada ya sherehe ya utalii Jumatatu nilisafiri kwenda California kuzindua kampuni ya utalii ya Tanzania Safari And Tourism inayomilikiwa na balozi wa heshima Ahmed Issa na sikurudi tena Washington, DC mpaka siku niliyoondioka"

Aliingia ndani zaidi kukana madai ya kutoka na star huyo wa filamu kwa kusema "sikuwahi kutanua na msanii huyu kama ilivyodaiwa lakini sishangai kwani mambo haya yamekuwa yakifanywa na genge la watu ambao miongoni mwao ni viongozi wa serikali na waliomo kwenye wizara yangu"

"Huyo Aunty nimezoea kumuona au kumsikia kwa kupitia vyombo vya habari lakini kwa mtazamo wa watu hawa wanataka kumfanya kiongozi atakapofika kwenye mkutano wowote ule na kumkuta mdada maarufu basi akimbie" Alisema Nyalandu ambaye mkewe Faraja Kota aliyetwaa taji la Miss Tanzania hiyo ni msomi pia huku akiwa hana skendo za ajabu ajabu kama baadhi ya mamiss wengine

Nyalandu alisema kuwa tayari amewatambua watu hao na kwamba yeye ataendelea na msimamo wake wa kulinda maslahi ya taifa hususani katika nafasi yake hiyo

                                                 Nyalandu na mkewe Faraja Kota
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment