Ile filamu kubwa kabisa kutengenezwa katika viunga vya Tanzania ya TmT movie imeanza maandalizi yake kwa kurekodi filamu mpya huku wasanii waliopatikana kutokana na shindano la Tanzania Movie Talent kuibeba sinema hiyo wakiwashirikisha wasanii wengine waliochaguliwa katika sinema hiyo.
Akiongea na Filamucentral mratibu wa filamu hiyo Staford Kihore amesema kuwa moja ya malengo makubwa ya Proin Promotions ni kuwajenga wasanii wa filamu na kuwapa uwezo wa kuigiza na kufanya kazi kimataifa, katika kuwasimamia wameanza nao kurekodi sinema TMT Movie.
“Tasnia ipo na inafanya vizuri lakini inahitaji uthubutu kwa kati ya wanaotengeneza sinema wawe tayari kufanya kitu kizuri kinachoweza kuvuka mipaka ndio tunachokifanya sasa baada ya kuwatengeneza kitaaluma wanafanya kazi,”anasema Staford.
Wasanii wa TMT wamefundishwa na kuiva katika fani ya uigizaji na moja ya alama yao wanayojivunia ni pale ambapo wamepewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao kupitia filamu ya TMT Movie na kuonyesha kile wanachoongea kwa watazamaji na wapenzi wa filamu Swahiliwood.
Filamu kubwa ya Tmt Movie inatarajiwa kuonyeshwa katika majumba ya Sinema Afrika Mashariki na Ulaya pia sinema inaongozwa na Muongozaji mahiri wa filamu Karabani na imeandikwa na Novatus Mgulusi ‘Ras Nova’ zaidi ya wasanii 200 kushiriki katika filamu hiyo.
Starring wa sinema hiyo ni milionia wa kutoka Mtwara Mwanaafa Mwizango na nyota wote wa TMT, huku wasanii nyota kibao kutoka tasnia ya filamu Tanzania wakipatia nafasi za ushiriki wa filamu hiyo inayojenga ajira kwa jamii nzima.
No comments:
Post a Comment