Monday, May 26, 2014

Mtunisy Arudisha Fadhila ITV, Kuonekana Leo Usiku Kwenye Taarifa Ya Habari.

Mtunisy
Nguli wa filamu nchini Nice Mohamed "Mtunisy" ni mmoja wa watu maarufu walioalikwa na kituo maarufu cha ITV ambacho kinaadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake. Kituo hicho kimemualika mtunisy katika sherehe zake hizo kama msanii ambaye alikuwa michezo yao toka Kaole Sanaa Group ilikuwa ikionyeshwa ITV. Mtunisy ataonekana katika habari za michezo na burudani  akizungumzia machache kuhusu sanaa ya filamu.
Swahiliworldplanet ilipomuendea hewani Star huyo anayekimbiza sokoni kwa sasa na filamu ya Tom Boy akiwa na Jackline Wolper alisema "Nilialikwa I.T.V kutoa shukrani Kwa kutimiza miaka 20 toka ianzishwe hivyo iliniita nikiwa Kama msaniiI niliyekuwa naonekana ITV kupitia michezo yetu ya KAOLE nami nimejaribu kurudisha fadhila Kwa kuwashukuru na kuwapelekea baadhi ya film zangu ambazo nimezifanya kupitia kampuni yangu ya Nice Entertainment na kuwashukuru wao Kwani bila ITV watu wasingemjua Mtunisy, nao wakanipa nafasi ya kuongea machache na itarushwa kwenye taarifa ya habariI ya Leo usiku"
Mtunisy

Filamu ya Tom Boy tayari ipo madukani nunua nakala yako halisi sasa.

No comments:

Post a Comment