Monday, May 26, 2014

Uzuri Wa Jackline Wolper Wamnyima Usingizi Kijana Huyu Mkenya.

Mara nyingi mashabiki hupenda kazi za mastaa aidha wawe wa filamu , muziki au fani nyingine kiasi cha kupelekea ushabiki wa kazi kwenda mbali zaidi kwa shabiki kutamani kuoana na star flani anayempenda. kwa wengi hubaki kuwa ndoto za alinacha hasa kutokana na watu wengi kuamini kuwa mastaa ni watu ghali sana kimaisha, kuanzia mavazi, misosi, usafiri na hata malazi na maisha yao ya kila siku hivyo wenye pesa pekee ndiyo hupata bahati ya kuwa nao. Wengine hujiozesha/kujifungisha ndoa na picha za mastaa wanaowapenda ilimradi tu kujifurahisha nafsi zao.

Jackiline Wolper
 Anyway, ni miezi kadhaa tangu nilipoanza kuchati na Edu Njuguna anayeonekana pichani ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Eldoret nchini Kenya . Edu ana kipaji cha muziki na anajichanga ili achomoke. Tangu siku ya kwanza na kila mara  nikichat nae lazima asifie filamu na uzuri wa star mkubwa wa filamu nchini Tanzania Jackline Wolper. Kwa mujibu wa Edu mwenyewe anapenda sana kuangalia filamu za Wolper na mojawapo anazozipenda ni Ndoa Yangu akiwa na marehemu Steven Kanumba, Edu pia aliwahi kusema kuwa anakubali sana filamu za Monalisa ingawa kwa Wolper amedata hasa kwa uzuri na urembo wa Wolper anapomuona kwenye Tv. Hata hivyo Wolper mwenyewe hana hili wala lile kuwa kuna mashabiki wake hawalali kwa kuteswa na uzuri wake na kuangalia filamu zake muda mwingi. Edu amesema kuwa akishakuwa tajiri na maarufu kupitia muziki itakuwa rahisi kumkaribia Wolper kuliko sasa!  lol.....very funny !

Itakuwa mara moja moja tunaweka hapa hisia za mashabiki kuhusu mastaa wao wanaowapenda kama hivi kwasababu wao hupata inspiration ya kuwa kama hao mastaa baadaye kwa wengine kuwa na vipaji na mengineyo, pia mashabiki hao hao ndiyo wasomaji wetu wakubwa na itawasaidia kuondoa stress kwa kuutua mzigo toka mioyoni mwao. Usisahau pia kuwa mastaa wengi mara kwa mara wanaingia kwenye hii blog na kusoma habari mpya kwasababu wao pia wanapenda updates kama watu wa kawaida.

No comments:

Post a Comment