Monday, May 26, 2014

Breaking News: Muigizaji Wa Filamu Nchini Rachel Haule Afariki Dunia.

Rachel Haule
Habari zilizotufikia muda huu ni kuwa muigizaji  wa filamu nchini Rachel Haule amefariki dunia asubuhi hii. Chanzo kimoja kilicho karibu na muigizaji mmoja ambaye ni rafiki wa karibu na Rachel kimeimbia SWP kuwa Rachel amefariki wakati akijifungua na mtoto pia amefariki. Alijifungua kwa operasheni katika hospitali ya taifa Muhimbili usiku wa kuamkia leo mtoto akafariki lakini baadaye na yeye akazidiwa na kuhamishiwa ICU ambapo alipoteza maisha asubuhi ya leo. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Ameen

Hili ni pigo jingine kwenye tasnia ya filamu nchini ambapoi wiki iliyopita ilimpoteza Adam Kuambiana.
Moja ya filamu za hivi karibuni ambayo ameigiza na pia kuitengeneza Rachel inaitwa Vanessa In Dilemma.
Rachel Haule


No comments:

Post a Comment