Muigizaji maarufu wa filamu Swahiliwood Halima Yahaya(Davina) amesema kuwa anataka kupata mtoto mwingine haraka kabla ya aliyemzaa miezi ya karibuni hajawa mkubwa ili amalizane na kazi ya ulezi na ajikite zaidi katika kazi zake za filamu. "unajua nimeona kuwa kulea siyo kitu cha muda mchache hivyo unatakiwa umalize kwanza ndiyo uendelee na kazi zako ambapo nimeona ni bora nitafute mwingine haraka haraka ndipo nijikite katika filamu" alisema Davina akizungumza na Globalpublishers.
Davina ameigiza filamu nyingi na hivi karibuni filamu yake mpya ya Sababu Ya Nasra akiwa na Slim Omar iliingia sokoni na kwasasa yupo location akishuti filamu mpya na King Majuto, Jenifer Kyaka(Odama) na Rachel Haule.
Davina
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news
No comments:
Post a Comment