Monday, April 21, 2014

Sina Kawaida Ya Kutoka Kimapenzi Na Kila Msichana: Tino

Tino
Star mkubwa wa filamu Swahiliwood Hisani Muya "Tino" amesema kuwa hana tabia ta kuwapanga wasichana au wasanii wenzake wa kike kwa kutoka nao kimapenzi na wanaomzushia hivyo wamekosa ya kufanya. Akizungumza na Filamucentral "Kiukweli nawashangaa sana hao wanaoniambia hivyo mimi sina tabia hiyo na wala sina muda wa kumpanga mtu kwangu, labda wananitaka sasa wanaona wazue hili ili waweze kunipata wamechemsha"

"Unajua watu wakikosa yakufanya huwa wanatafuta sababu ya kukuchafua ili uonekane mbaya kwa mashabiki, naomba waniache nifanye kazi kwenye sanaa niliingia muda mrefu sana kama ni kuwapanga mstari nilishindwa kipindi hicho sasa leo nitawezaje, hao hawana lolote la maana wanataka kuonekana kwenye vyombo vya habari kwasababu wamesha poteza umaarufu kwa mashabiki hivyo wanatafuta njia ya kujirudisha" alisema Tino ambaye anakimbiza sokoni na filamu mbalimbali huku akiwa mmoja wa waigizaji wa kiume wenye uwezo mkubwa wa kuigiza na kubadilika kulingana na character.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni tarehe 24 April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment