Saturday, June 29, 2013

GEOFREY KUSILA, MUIGIZAJI WA FILAMU ANAYEKUJA JUU KWA KASI.

Geofrey Kusila ni muigizaji wa filamu anayekuja juu hivi sasa , anatarajia kuingiza sokoni muda si mrefu filamu mbili ambazo ni Ndoa Goli La Tatu ambayo yupo na Nuru Nasor(Nora), Slim Omar na Shamsa Ford, Pia filamu yake ya Cest La Vie itaingia sokoni muda si mrefu. Kusila amesema kuwa mwishoni mwa mwaka huu anakuja na project kubwa ingawa hakutaka kuiweka wazi kwasasa.

Muigizaji huyo pia anafanya kazi kama production manager wa kampuni ya Leo Media inayohusika na usambazaji wa filamu za kiswahili. Kusila alianza sanaa mwaka 2000 na amepitia makundi mengi ya sanaa na kufanya kazi pamoja na wasanii kama Cloud, Jenifer Kyaka(Odama), Suleiman Barafu na Slim Omar. Alicheza katika filamu ya Security akiwa na Cloud na baada ya hapo alienda nje ya nchi na baadaye kurudi na filamu ya Facebook aliyotengeneza Uingereza. Baadaye alishiriki filamu ya Kashfa halafu akatoa yake nyingine ya Mchana wa Kiza. 

           Geofrey Kusila akimkabidhi Mboto mkataba baada ya kumsainisha na kampuni ya Leo Media.

No comments:

Post a Comment