Slim aliyasema hayo baada ya Swahiliworldplanet kumuuliza kuwa hapati usumbufu kutoka kwa wasichana baada ya kuwa maarufu na ni kwanini akaunti yake facebook haipo kwasasa?, ndipo alipofunguka muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto unaowadatisha wanawake wengi wa mjini. Alisema kuwa baadhi ya watu wanatumia vibaya mitandao ya kijamii wakati inatumiwa na watu wa rika zote."ntarudi 2 ndugu yangu nimetoka kwa muda maana kuna baadhi ya kina dada walikuwa wanai2mia vbaya kama unavyojua mitandao ya kijamii wanatazama wa2 wa kila rika na usumbufu upo kwa kna dada na ngumu kuzuia hisia zao na vibaya kuwajibu maneno mabaya ndo maana nimejitoa kwa muda ila ntarudi soon"
Muigizaji huyo anaonekana katika filamu kama vile Waves of Sorrow, I am Lost, Family War, Kivuli na nyinginezo huku filamu zake nyingine mpya zikitarajiwa kuwa sokoni muda si mrefu.
No comments:
Post a Comment