NB: (Mpaka ukimaliza kusoma makala yote hapa nafikiri utakuwa umeelewa vizuri).
Mpaka sasa fashion industry ya Tanzania kidogo imeonyesha mwanga lakini baadhi ya madizaina,wanamitindo na wadau wa fashion wanaonekana kutoona umuhimu wa kuwa na umoja wa kuwaleta pamoja ili kuishinikiza na kuishawishi serikali itoe sapoti yake na kuwa sector rasmi ili kuongeza ajira zaidi na kukuza ubunifu wa mitindo nchini tafauti na ilivyo sasa madizaina wapo kienyeji zaidi na kubaki kulalamika. Pia ni muhimu kupigania sera ya mitindo na ubunifu nchini ambayo kwa sasa inaonekana kutokuwepo. Sera ya fashion ni muhimu sana na ipo hata kwa nchi zilizoendelea kwenye mitindo duniani ili industry ikubalike serikalini kama sekta rasmi ili kuwa rahisi kwa serikali kusaidia tasnia hiyo kupitia bajeti yake ya kila mwaka maana ndani ya sera kila kitu kitakuwa wazi ukiwemo wajibu wa serikali katika tasnia hiyo.
Madizaina na models kila siku wanalalamika na kutaka wasaidiwe lakini hawana umoja na hawajui kuwa sera ya fashion ni muhimu sana ili tasnia ikuwe na sio kufanya fashion shows pekee. Niseme wazi kuwa madizaina wengi wa Tanzania na wanamitindo na hata baadhi ya wanaoandika kuhusu fashion na mitindo nchini hawajui kuwa kutokuwepo kwa sera ya ubunifu wa mitindo ni moja ya vikwazo vikubwa kwa kutosaidiwa na serikali na hakuna mwingine wa kuipigania sera hiyo bali madizaina wenyewe na wanamitindo wanatakiwa kuunda umoja sasa wa kuwakutanisha wote kwa pamoja ili kuwe na sauti moja yenye nguvu ili kuishinikiza serikali itambue fashion industry kama sector rasmi. kama kutakuwa na vyama vingine vidogo vidogo kama vya madizaina pekee, models peke yao na wengineo hiyo inatakiwa iwe baadaye lakini siyo sasa. Umoja wa models Tz upo lakini chanzo cha kuaminika kimesema kuwa wanamitindo wenyewe hawapo active kama wapo wapo tu kitu ambacho ni tatizo kubwa. Ndio linaweza kuundwa shirikisho la mitindo nchini kama ilivyo katika films ambapo serikali imeanza harakati za kukuza tasnia ya filamu baada ya wadau kuunda umoja wao hivyo kuwa rahisi kwa serikali kusaidia.
Nchi zote unazoziona zimeendelea katika fashion industry zimefanya yote haya na sio kama tunavyoona madizana na models wakipita jukwaani tu ukajua ndiyo kukuza fashion industry. Sera za mitindo zimepiganiwa na wadau wa nchi hizo wenyewe na sio London, Paris, Milan au New York fashion weeks pekee zilizokuza fashion nchi hizo bali serikali pia kupitia sera ya mitindo . Sera ni kama msingi wa nyumba au muongozo wa kitu chochote kile ikiwa nzuri maendeleo yatakuwepo ikiwa mbaya au isipokuwepo hakuna kitu. wadau wanatakiwa waunde umoja imara tena kwa wakati huu ni kitu muhimu sana maana rais Kikwete ni rais pekee ambaye ameonyesha kupenda na kuisapoti michezo na burudani nchini ili mpaka akimaliza muda wake wa uongozi mwaka 2015 basi tasnia itakuwa imepata muelekeo na rais anayekuja anatakiwa kukamilisha tu au kumalizia ya mtangulizi wake lakini kama bado wabunifu na models watakuwa usingizini kwa kutokuona umuhimu wa kuwa na umoja imara na kupigania sera ya mitindo nchini basi tasnia hii haitakuja kutambulika serikalini kama sector rasmi hata siku moja. Niseme tu kuwa kufanya fashion shows kila siku au kila mwezi ni kitu muhimu ili tasnia ikue but mbunifu mmoja hata afanye shows ulaya na marekani kila siku na mastaa wote wa Hollywood wahudhurie shows zake kamwe hawezi kuishawishi serikali itambue tasnia hii kama sector rasmi bali kupitia umoja ambao utakuwa na members na viongozi watakaokaa na viongozi wa serikali na kufanya follow up kila siku.
Kabla sijaandika hapa niliwauliza madizaina sita hasa nikilenga wenye majina kati yao 4 walinijibu vizuri na kwa ushirikiano mzuri lakini wawili hawakujibu mpaka naandika hapa. Madizaina wawili walienda mbali zaidi kwa kusema kuwa baadhi ya madizaina wanajiona wana majina kuliko wenzao so hawaoni umuhimu wa umoja. madizaina wengine wawili pia karibia wote walitoa jibu moja kwa kusema huwezi sema Tanzania Mitindo House ni umoja wa madizaina maana umeanzishwa na mtu mmoja so hata malengo yake siyo ya kuwainua madizaina na wanamitindo bali ya kuikuza taasisi hiyo inayosaidia watoto walio katika mazingira magumu.
Sera ikipiganiwa mambo muhimu na kila kitu kitakuwa wazi ikiwemo kuondoa migongano na mitafaruku ya baadaye mfano madizaina wengine now wanaweza kuwa na malengo ya kuanzisha Fashion Weeks au Fashion awards lakini kutokana na kutokuwa na sera au muongozo wa mitindo nchini kunaweza kutokea migongano au kutofautiana na waandaaji wa Swahili Fashion Week wakidai kuwa categories zao za tuzo za fashion au fashion weeks zao zinafanana na Swahili Fashion week au hata shows zingine kutoka kwa madizaina wengi chanzo kikiwa ukosefu wa sera ya mitindo. kwa ufupi kupitia sera ya mitindo(policy)......
1.Serikali itaitambua tasnia hii na hivyo kutengewa bajeti yake kila mwaka kwa ajili ya kujenga viwanda vya malighafi za mitindo kama vile vitambaa na ngozi ambavyo kwa sasa hakuna hivyo kuwa gharama kwa madizaina kununua toka nje.
2.Serikali pia itaweka sera kuhusu soko la bidhaa za wabunifu wa ndani ili wapewe kipaumbele kama wenzao wa nje. serikali pia miaka michache ijayo kupitia sera nzuri inaweza kuanza kuzuia uingizaji wa nguo, viatu na vitu vingine toka kwa wabunifu wa nje na hatimaye miaka mingine baadaye kukomesha kabisa importation na kuhimiza exportation kwa wabunifu wa nchini.
3.Kupitia sera nzuri pia wafanyakazi wa serikali na viongozi wa kiserikali wanaweza kuwa mfano mzuri kwa kuvaa nguo za wabunifu wa Tanzania popte pale kama moja ya mikakati ya serikali kukuza na kuwainua wabunifu wa ndani.
4.Kupitia sera nzuri serikali inaweza kuwatumia wanamitindo katika matangazo ya taasisi zake mbalimbali na pia makampuni makubwa kama ya simu, bank na nyinginezo kutumia wanamitindo chini ya umoja wao na sio kuchukua kila mtu kiholela hata wasio na sifa kama ilivyo sasa.
5.Pia wanamitindo wapewe heshima yao kutokana na kazi zao na sio kama ilivyo sasa hata mwamitindo wa kimataifa wa tanzania akienda katika taasisi za serikali au mashirika makubwa ili kuanzisha vitu vya msingi kwa jamii kama vile NGO anasumbuliwa na kukumbana na urasimu mpaka inachosha kama si aibu kwa taasisi hizo ni kwa kuwa tasnia hii haitambuliki serikalini.
6.Pia kupitia umoja na sera nzuri ukiachilia mbali madizaina binafsi kuanzisha fashion weeks binafsi lakini umoja huu unaweza kuwa na fashion week yake ambayo inamilikiwa na madizaina wote ili kutangaza kazi zao na kuzidi kuinua vipaji vipya na pia kuanzisha tuzo za mitindo.
7.Kupitia sera nzuri serikali inaweza kuwa mfano wa kwanza kudhamini fashion weeks zitakazofanyika nchini na show za wabunifu ili kuwapa moyo, pia serikali ishawishi makampunim binafsi yadhamini shows za mitindo tofauti na ilivyo sasa udhamini ni shida au ni kwa kuangaliana kwa majina.
"Hayo ni maoni hakuna chuki na mtu ili kuzidi kusonga mbele"
"UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU"
ahsanteni
Some of Tanzania designers
No comments:
Post a Comment