Kuna baadhi ya maswali yanaibuka kutoka kwa mashabiki wa muigizaji mkubwa nchini Salma Jabu Nisha kuwa ni kwanini hana mabifu na wasanii wenzake kama baadhi ya masataa wenzake walivyo. Nisha amejibu hayo kwa kusema ...
"wacha niwaambie kitu mashabiki wangu kwamba mimi nimefunzwa maadili na mama yangu na pia nina washauri wazuri sana katika maisha yangu, mara nyingi huwa siwezi kugombana na mtu kisha nikamtangaza, kugombana ni kawaida lakini sio kutangaza hovyo kwamba nina ugomvi na mtu fulani then huwa mwepesi wa kusamehe, huwa napenda ushindani wa kazi bora na kibiashara lakini sio kulumbana bila sababu au kuchukiana hovyo, ndivyo nilivyo" Alisema Nisha aliyejaaliwa uzuri na macho yenye mvuto wa kimapenzi.
No comments:
Post a Comment