Thursday, February 27, 2014

Watanzania Mpaka Wamuone Mzungu Akisifia Sanaa Na Wasanii Wa Tanzania Ndiyo Na Wao Wasifie: Yuster Nyakachaka

Yuster
Muigizaji wa filamu nchini Yuster Nyakachaka ambaye pia ni mwanamuziki wa nyimbo za asili kupitia kundi la Dar Creators amesema kuwa huwa anasikitishwa na baadhi ya watanzania kutopenda sanaa za Tanzania badala yake wao huwa watu wa kuponda muda wote lakini pale wanapomuona mzungu akishabikia sanaaa ya Tanzania na wao ndiyo huanza kushabikia kitu ambacho ni kama utumwa mambo leo.

 Akizungumza na Filamucentral star huyo wa filamu za Oysterbay na Majuto Si Hasara inayotarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni alisema "Kila mtu anakubali kuwa filamu zetu za Kibongo zinakubalika lakini watu hawataki kujionyesha kama wanapenda vitu vya nyumbani, hiyo ni tabia ya watanzania hawakukubali hadi waone labda wazungu wakishabikia kazi zetu"



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment