Navutiwa Zaidi Na Wanaume Weusi na Sio Weupe: Wema Sepetu
|
Wema Sepetu |
Wema Sepetu amesema kuwa yeye mzuka wake upo kwa wanaume weusi zaidi na sio wanaume weupe. Akizungumza kwenye kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na radio Clouds Fm Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 ambaye pia ni star wa filamu Swahiliwood aliulizwa mwanaume mwenye sifa gani anayevutiwa nae na kuweza kumuoa, Wema alijibu "Kuolewa sio shida je huyo mwanaume nampenda,maana naweza kuja kuchumbiwa lakini nisimpende, Mimi nampenda Mwanaume mweusi,wanaume weupe sio kwamba sijawahi kuwa nao lakini nakuwa sina mzuka nao"
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake wa kimapenzi na Diamond Platinumz mrembo huyo asiyekauka kwenye media alisema " Kweli niko na Nasib - Diamond na nadhani muda huu kutakua na
utulivu ndani yake,ule utoto tuliokua tunafanya nadhani ulikuwa utoto na
imekua Power Couple toka mwaka 2010 kwa hiyo tuna ni miaka 4 sasa,kwa
sasa tumeamua kuwa serious"
Wema na Diamond
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news, life styles news and more
No comments:
Post a Comment