Friday, June 13, 2014

Nando Amenikera Sana, Anataka Kiki Kupitia Jina Langu: Lulu

Lulu
Star wa filamu Swahiliwood Elizabeth Michael "Lulu"  amesema kuwa amekerwa na kitendo cha Nando kusema kuwa aliwahi kuwa mpenzi wake. Akizungumza na Globalpublishers Lulu amesema kuwa ni kweli Nando aliwahi kumtokea na kumkubalia lakini hawakufanya lolote yaani kama wapenzi kwakuwa alimgundua mapema Nando kuwa hakuwa na nia nzuri kwake na alikuwa anataka kiki kupitia yeye

"Nahisi Nando alikuwa kwanza anataka kiki kupitia mimi na ndiyo maana kila alipotaka kupiga picha na mimi, nilimkatalia coz nilishamgundua nia yake, nimemshangaa kweli alipotangaza kuwa niliwahi kuwa mpenzi wake labda alivyonitokea na kumkubalia lakini sikufanya naye chochote kinachohusu mapenzi ndiyo akaona aseme hivyo"
Nando
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment