Pages

Tuesday, May 7, 2013

HUYU NDIYE SUPERSTAR WA KWANZA WA KIKE NA KIUME KATIKA HISTORIA YA MIAKA 100 YA BOLLYWOOD.

India inaadhimisha miaka 100 tangu kutengenezwa kwa filamu ya kwanza huku miaka mingi ikitengeneza mastaa wengi wakubwa waliojulikana na kupata heshima mpaka kwa wazungu Hollywood. Ukweli ni kuwa wapo superstars wengi wa Bollywood kama vile Amitabh Bachchan, Shahrukh Khan, Aamir Khan, Salman Khan, Dilip Kumar, Raj Kapoor, Dharmendra, Hrithik Roshan, Rish Kapoor na wengine wengi kwa upande wa wanaume. Lakini Rajesh Khanna(1942-2012) ndiye anaaminika kuwa superstar wa kwanza halisi wa Filamu za Bollywood akipata hadhi hiyo kutokana na kazi zake zilizokubalika sana kwa film critics na kufanya vizuri sana sokoni kiasi cha kuweka rekodi kadhaa ambazo nyingine mpaka leo bado kuvunjwa. amepata tuzo nyingi sana kama muigizaji bora. Alianza kuigiza mwaka 1966 baada ya kushinda shindano la kutafuta vipaji.

 Kabla yake walikuwepo mastaa wakubwa wa filamu lakini ujio wake ulikuwa tishio. Alikuwa na mashabiki wengi sana hasa wanawake wengi wakimuandikia barua kwa damu zao baada ya kujikata kusudi huku wanawake wengine wakijiozesha kwa kutumia picha zake. Hata waigizaji wenzake mastaa wakubwa kipindi hicho wakiwemo Sharmila Tagore na Mumtaz walikiri kuwa hawakuwa kitu mbele ya Rajesh walipoongozana nae. Rajesh alimuoa Dimple Kapadia ambaye pia ni actress maarufu sana Bollywood na walipata watoto wawili akiwemo Twinkle Khanna aliyeolewa na Akshay Kumar. Rajesh alifariki mwaka 2012. Alikuwa muigizaji anayelipwa sana kuanzia mwaka 1970-1979. Amitabh Bachchan pia aliwahi kukiri kuwa Rajesh ni funga kazi.  Mastaa wengine wa sasa na wanaochipukia mara nyingi humtaja kama inspiration ya wao kuwa waigizaji. Baadhi ya filamu zake zilizompatia umaarufu mkubwa ni pamoja na Aradhana, Raaz, Ittefaq, Kudrat, Bandish. Muangalie superstar wa kwanza wa kike Bollywood hapo chini............

                                                Rajesh Khanna enzi zake akitamba

Kwa upande wa waigizaji wa kike wa Bollywood Sridevi(49) ndiye anayekubalika kuwa superstar wa kwanza wa kike wa filamu za kihindi kutokana na kuacha historia katika filamu hizo. Kabla yake alitanguliwa na waigizaji wa kike wengi waliopata mafanikio makubwa kama vile Madhubala, Waheeda Rehman, Sharmila Tagore, Rekha, Hema Malini, Jaya Bachchan, Nargis, Mumtaz na wengineo lakini ujio wa Sridevi aliyejaaliwa uzuri na kipaji cha pekee ikawa story mpya katika filamu za Bollywood. umaarufu wake ulitokana na kazi na siyo skendo. Inasemekana kuwa waandishi kibao walikuwa wakitunga story na kuandika script lakini akilini mwao wakimfikiria Sridev katika characters hizo. Sridevi amecheza filamu nyingi sana za lugha mbalimbali na kufanikiwa sana critically na kimauzo lakini lugha nyingine alizotumia kucheza filamu hizo hazijui mpaka leo.

Baadhi ya filamu zilizompa umaarufu mkubwa ni pamoja na Sadma, Chandni, Gumrah, Judaai, Lamhe, Khudah Gawah, Nagina na English Vinglish iliyotoka mwaka 2012. Alianza kuigiza tangu akiwa mtoto mwaka 1967 na ndiye mwigizaji wa kike aliyekuwa namba 1 miaka ya 1980. anaaminika kuwa mmoja wa waigizaji waliotamba sana katika sinema za kihindi kwa muda mrefu na kuwa na mfanikio makubwa hata baada ya umri kuanza kumtupa lakini alirudi mwaka 2012 kama muigizaji mkuu katika filamu ya English Vinglish na kufanikiwa sana baada ya kuwa nje ya filamu kwa miaka 15 mfululizo. Sridevi alianza kutetemeshwa na ujio wa muigizaji mwingine hatari Madhuri Dixt aliyechukua nafasi yake baadaye kama muigizaji namba moja. Leo wapo masupastaa wakubwa wa kike wa Bollywood kama vile Aishwarya Rai, Kajol, Kareena Kapoor, Rani Mukerjee na wengineo lakini walitanguliwa na Sridevi na wengine wakishindwa kufika level yake licha ya kuwa maarufu sana kwa kazi zao.

                                                     Sridevi(49) alivyo sasa





No comments:

Post a Comment