India inaadhimisha miaka 100 tangu kutengenezwa kwa filamu ya kwanza
huku miaka mingi ikitengeneza mastaa wengi wakubwa waliojulikana na
kupata heshima mpaka kwa wazungu Hollywood. Ukweli ni kuwa wapo
superstars wengi wa Bollywood kama vile Amitabh Bachchan, Shahrukh Khan,
Aamir Khan, Salman Khan, Dilip Kumar, Raj Kapoor, Dharmendra, Hrithik
Roshan, Rish Kapoor na wengine wengi kwa upande wa wanaume. Lakini
Rajesh Khanna(1942-2012) ndiye anaaminika kuwa superstar wa kwanza
halisi wa Filamu za Bollywood akipata hadhi hiyo kutokana na kazi zake
zilizokubalika sana kwa film critics na kufanya vizuri sana sokoni kiasi
cha kuweka rekodi kadhaa ambazo nyingine mpaka leo bado kuvunjwa.
amepata tuzo nyingi sana kama muigizaji bora. Alianza kuigiza mwaka 1966
baada ya kushinda shindano la kutafuta vipaji.
Kabla
yake walikuwepo mastaa wakubwa wa filamu lakini ujio wake ulikuwa
tishio. Alikuwa na mashabiki wengi sana hasa wanawake wengi
wakimuandikia barua kwa damu zao baada ya kujikata kusudi huku wanawake
wengine wakijiozesha kwa kutumia picha zake. Hata waigizaji wenzake
mastaa wakubwa kipindi hicho wakiwemo Sharmila Tagore na Mumtaz walikiri
kuwa hawakuwa kitu mbele ya Rajesh walipoongozana nae. Rajesh alimuoa
Dimple Kapadia ambaye pia ni actress maarufu sana Bollywood na walipata
watoto wawili akiwemo Twinkle Khanna aliyeolewa na Akshay Kumar. Rajesh
alifariki mwaka 2012. Alikuwa muigizaji anayelipwa sana kuanzia mwaka
1970-1979. Amitabh Bachchan pia aliwahi kukiri kuwa Rajesh ni funga
kazi. Mastaa wengine wa sasa na wanaochipukia mara nyingi humtaja kama
inspiration ya wao kuwa waigizaji. Baadhi ya filamu zake zilizompatia
umaarufu mkubwa ni pamoja na Aradhana, Raaz, Ittefaq, Kudrat, Bandish.
Muangalie superstar wa kwanza wa kike Bollywood hapo chini............
Rajesh Khanna enzi zake akitamba
Kwa
upande wa waigizaji wa kike wa Bollywood Sridevi(49) ndiye
anayekubalika kuwa superstar wa kwanza wa kike wa filamu za kihindi
kutokana na kuacha historia katika filamu hizo. Kabla yake alitanguliwa
na waigizaji wa kike wengi waliopata mafanikio makubwa kama vile
Madhubala, Waheeda Rehman, Sharmila Tagore, Rekha, Hema Malini, Jaya
Bachchan, Nargis, Mumtaz na wengineo lakini ujio wa Sridevi aliyejaaliwa
uzuri na kipaji cha pekee ikawa story mpya katika filamu za Bollywood.
umaarufu wake ulitokana na kazi na siyo skendo. Inasemekana kuwa
waandishi kibao walikuwa wakitunga story na kuandika script lakini
akilini mwao wakimfikiria Sridev katika characters hizo. Sridevi
amecheza filamu nyingi sana za lugha mbalimbali na kufanikiwa sana
critically na kimauzo lakini lugha nyingine alizotumia kucheza filamu
hizo hazijui mpaka leo.
Baadhi ya filamu zilizompa
umaarufu mkubwa ni pamoja na Sadma, Chandni, Gumrah, Judaai, Lamhe,
Khudah Gawah, Nagina na English Vinglish iliyotoka mwaka 2012. Alianza
kuigiza tangu akiwa mtoto mwaka 1967 na ndiye mwigizaji wa kike
aliyekuwa namba 1 miaka ya 1980. anaaminika kuwa mmoja wa waigizaji
waliotamba sana katika sinema za kihindi kwa muda mrefu na kuwa na
mfanikio makubwa hata baada ya umri kuanza kumtupa lakini alirudi mwaka
2012 kama muigizaji mkuu katika filamu ya English Vinglish na kufanikiwa
sana baada ya kuwa nje ya filamu kwa miaka 15 mfululizo. Sridevi
alianza kutetemeshwa na ujio wa muigizaji mwingine hatari Madhuri Dixt
aliyechukua nafasi yake baadaye kama muigizaji namba moja. Leo wapo
masupastaa wakubwa wa kike wa Bollywood kama vile Aishwarya Rai, Kajol,
Kareena Kapoor, Rani Mukerjee na wengineo lakini walitanguliwa na
Sridevi na wengine wakishindwa kufika level yake licha ya kuwa maarufu
sana kwa kazi zao.
Sridevi(49) alivyo sasa
No comments:
Post a Comment