Pages

Tuesday, May 7, 2013

OMOTOLA NA MEL B WA SPICE GIRLS WAWA MASHOSTITO, GENEVIEVE NNAJI LIVE SHOW YA BEYONCE LONDON.

Nollywood superstar Genevieve Nnaji ameenda kuangalia live show ya Beyonce akiwa sehemu ya V.I.P huko London ambapo Beyonce anaendelea na tour yake ya muziki nchi mbalimbali. Mtoto wa Beyonce Blue Ivy inadaiwa pia alipanda jukwaani na kuvuta umati wa watu. show hiyo ilijaza watu sana. Kwa upande mwingine nako superstar mwingine wa Nollywood Omotola Jalade nae bado yupo Marekani huku akila bata na mastaa wakubwa wa huko akiwemo Mel B wa kundi la Spice girls. Pia juzi kati Omotola alikuwa na Michele Williams wa Destitny Child. Hivi karibuni Omotola alitajwa kama mmoja wa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani na jarida la Time Magazine na kualikwa kwenda marekani kukutana na mastaa wengine waliotajwa katika orodha hiyo.

                                                            Genevieve Nnaji kulia

                                                            Omotola with Mel B



No comments:

Post a Comment