Pages

Wednesday, May 8, 2013

ISABELA MPANDA KUJA NA JIKUBALI, JOKATE KUDIZAINI MAVAZI YAKE.

Isabela Mpanda ambaye ni actress na mwanamuziki wa Bongofleva anakuja na wimbo mpya wa Jikubali nje ya kundi lao la Scorpion Girls akiwa na Jackline Pentezel na Miriam Jolwa(Jini Kabula).Isabela alipoulizwa na SWP ni kwanini amaeamua kuja peke yake na wimbo wa Jikubali bila kuwashirikisha wenzake alisema kuwa ameamua kuwaonyesha mashabiki wake kuwa anaweza kusimama peke yake si lazima awe na kundi lake. Wimbo huo umerekodiwa Natal Records, video ya wimbo huo itatengenezwa na Adam Juma wa Visual Lab na costume designer atakuwa Jokate a.k.a Kidoti. Isabela alisema "Nataka niwaonyeshe mashabik wangu kuwa naweza kusimama peke yangu siyo adi kundi. Wimbo wa kundi mpya tayar uko hewan Nchi Yetu. Na mimi nakuja na wimbo mpya unaitwa Jikubali kwanza mwenyewe. Nimefanya Natal record producer Abba process na mixing itafanyiwa ngoma record kwa Tudd thomas. Video nitashut kwa Adam Juma na mavazi kwa Joket. Kidot"

Kwa upande mwingine pia filamu aliyocheza Isabela inayoitwa Tatakoa inatarajiwa kuingia sokoni wiki ijayo. Filamu hiyo imeongozwa na Mr. Chuzi na washiriki wengine ni pamoja na Salma Jabu(Nisha), Rayuu, Zerish, Baby Madaha na wengineo.

No comments:

Post a Comment