Ramsey Hashim(Hashim Kambi) anakuja na filamu yake mpya ya Fisadais huku akiwa amemshirikisha Zahir Ally Zoro ambaye ni mwanamuziki mkongwe nchini na watoto wake Banana Zoro na Maunda Zoro nao wakiwa wanamuziki maarufu na kutupa kete zao katika filamu za Swahiliwood pia. Zahiri Ally Zoro atacheza kama mpelelezi katika filamu hiyo huku ikisubiriwa kwa hamu kubwa kama muonekano wake uliozoeleka kama mwanamuziki utabadilika kwakuwa ni lazima character yake itamtaka kubadilika kimuoekano ili kuendana na character hiyo ya upelelezi. Katika hiyo filamu wapo pia Hidaya Njaidi, Mboto na Ruth Suka(Mainda).
No comments:
Post a Comment