Monday, December 15, 2014

Diamond Platnumz Alaani Habari Kuwa Aliwadhalilisha Kina Nyota Ndogo.

Baada ya mtandao wa Standardmedia wa Kenya kuandika habari kuwa Diamond aliwadhalilisha Nyota Ndogo na Susumila kwa kudaiwa kuwafukuza VIP Lounge waliyokuwa wamepangiwa wote wakisubiri kutumuiza katika show.
Pia kudaiwa kuwanyima maji safi ya chupa na kuwataka wakanywe maji ya bomba Diamond amefunguka kulaani kitendo hicho akisema ni cha uongo na sio kizuri katika umoja wa wasanii wa Afrika mashariki. Kupitia akaunt zake za mitandao ua kijamii Diamond ameandika .......

Nimesikitishwa Sana na habari zilizoandikwa na moja ya chombo cha habari, kuwa eti nliwanyanyasa wasanii wenzangu Nyota ndogo na Susumila, kwa kuwafukuza kwenye VIP lounge na sijui eti niliwazuia wasitumie maji ya chupa hivi inaingia akilini kweli hii!!!?? Ningependa kutumia nafasi hii kuwajulisha mashabiki zangu waliokutana na story hizo kuwa sio za kweli ni zenye lengo la kudhoofisha Mahusiano yetu mazuri ya wasanii Wa Africa mashariki..kama BigEye ya Uganda ilivyowahi kuandika habari za upotoshaji Kati yangu na Jose Chameleone.. 

Pia Nawasihi @Bongofive ni vyema mtambue Nafasi yenu kwenye jamii kwa sasa, Kuweni makini na baadhi ya habari mnazo post ama kureport kutoka baadhi ya mitandao, zinavunja mahusiano mazuri ya wasanii wa East Africa...kumbukeni kuna watu wana tabia ya kujudge kitu kwa kusoma kichwa cha habari tu pasipo kufuatilia undani wa habari...Yawezakuwa mwaandika kwa nia njema tu, lakini ni vyema muwe mnapata na uhakika kwanza kabla ya kuripoti, hususan story za kutengeneza chuki kama hizi....kufanya hivyo ndiyo mtasaidia kukuza industry yetu ya East Africa...

Msanii Susumila pia amekana habari za kudhalilishwa na Diamond akisema ni majungu yamepikwa soma hapa Hatujadhalilishwa na Diamond: Susumila

No comments:

Post a Comment