Tuesday, November 4, 2014

Sitti Mtemvu Kuvuliwa Taji La Miss Tanzania 2014 Muda Wowote Kuanzia Sasa !

Sitti Mtemvu
Wakati serikali kupita Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ikisema itakifuta cheti cha kuzaliwa cha Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu,  taarifa zinasema kwamba hawezi tena kuendelea na taji hilo.
Imethibitisha kwamba uamuzi umekwisha kufanyika wa kumvua Sitti taji hilo alilovikwa katika mazingira tata, uamuzi unaotarajiwa kutangazwa wakati wowote kuanzia sasa.
Hata hivyo, haijafahamika kama hatua hiyo itachukuliwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ama Sitti mwenyewe baada ya kubainika kwamba taji hilo linazidi kuiweka pabaya familia ya Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, ambaye ni baba yake.

Imebainika kwamba hata hatua ya awali ya kuwania taji hilo ilichukuliwa na Sitti na baadhi ya wanafamilia bila kushirikishwa kwa Mbunge Mtemvu, jambo ambalo lilimsononesha awali katika ushiriki wa Miss Temeke.

Imefahamishwa kwamba Mbunge Mtemvu amekerwa na hali inayoendelea ikiwa ni pamoja na kuwapo utata wa cheti cha kuzaliwa cha mwanae Sitti, pamoja na kuwa anawajibika kisheria kwa anayoyafanya kutokana na kufikia umri wa zaidi ya miaka 18

No comments:

Post a Comment