Saturday, October 18, 2014

Timoth Conrad Atua Nchini Marekani Kwa Ajili Ya Tuzo Za Silicon Valley Film Awards 2014, Dogo Masai Kutamba ?

Mtengeneza filamu maarufu nchini Timoth Conrad ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Timamu African Media tayari ametua nchini Marekani kwa ajili ya tuzo za Silicon Valley African Film Festival ambapo filamu yake ya Dogo Masai imependekezwa kuwania Best Feauture film
ikichuana na filamu za S.Africa, Nigeria, Uganda, Misri na Malawi. Filamu hiyo ambayo ni filamu pekee toka Tanzania kuiwakilisha nchi katika tuzo hizo inatarajiwa kuonyeshwa Jumapili hii ambayo ndiyo usiku wake tuzo zinatolewa.

Dogo Masai imewakutanisha wasanii wenye vipaji nchini kama Omary Clayton, Kemmy Julieth Samson, Tino Hisani Muya

Kila la kheri Tico na team nzima ya watengezaji wa Dogo Masai. Angalia picha Tico akiwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere International Airport wakati alipoondoka kwenda Marekani....


No comments:

Post a Comment