Saturday, October 18, 2014

Happy Nyatawe Awachana Wasanii Wanaoishi Maisha Fake.

Happy Nyatawe
Muigizaji maarufu wa filamu nchini Happy Nyatawe ambaye anatarajiwa kuonekana katika filamu mpya ya Hakuna Matata akiwa na mastaa wenzake kama Nisha, King Majuto na Hemedy Suleiman, amesema kuwa baadhi ya wasanii wa filamu nchini wanapenda kuishi maisha ya kuigiza kwa kujifanya wana pesa sana kumbe holaa!.
Happya amesma kuwa baadhi yawasanii hukodisha magari ya kifahari na kutanulia nayo wakijifanya ni yao kwa kuogopa kupanda daladala kitu ambacho yeye ahawezi kukifanya kwani anapenda kujishughulisha na hapendi kujikweza.

Happy alisema "Wasanii wenzangu tusipende kuishi maisha ya kuigiza tuishi maisha yetu kama huna ipo siku Mungu atakupa ....usiogope kupanda daladala show off hazina mpango"

Alichokisema Happy kimekuwa kikisemwa pia na baadhi ya wasanii wenzake ambao hawapendi kujikweza kuwa kuna wasanii wengi wanajifanya maisha mazuri kumbe hakuna kitu

No comments:

Post a Comment