Saturday, October 25, 2014

Nina Uzoefu Miss Tanzania Kuna Ujanja ujanja Mwingi Kumpata Mshindi: Faiza Ally

Faiza Ally
Faiza Ally ambaye aliwahi kushiriki mashindano ya urembo ya Miss Tanzania miaka ya nyuma na ambaye pia kwasasa ni muigizaji wa filamu nchini. Ameamua nae kufunguka uzoefu wake kuhusu mashindano hayo wakati huu ambapo ushindi wa Sitti Mtemvu umekuwa hot topic kwenye media na social media kwa ujumla.
Faiza ameandika...........

"Naomba kidogo nizungumzie haya mambo ya miss Tanzania kutokana na uzoefu wangu kidogo...mm nilisha wahi kuwa miss Tabata number 3 na nikaenda Ilala na pia nilisha shiriki Mara kazaa Dodoma ... Kwa kifupi mimi sishangai sana kuhusu Sitti kupewa taji kwa njia ambayo si halali kwa sababu Mara nyingi warembo wanaoshinda huwa wanajijua na wanapangwa...

 Mfano mzuri baada ya mimi kushinda miss Tabata nilipoenda Ilala kalikumtima muandaaji aliniambia kuwa Kama ningekuwa karibu na waandaaji ningeshinda kwa kweli sijamuelewa kabisa kwa nini alitumia hiyo kauli... Pia mshindi wetu wa miss Tabata alikuwa anatembea na mdhamini wetu..

. Tatu kuna tofauti unaona hasa wakati wa mazoezi kuna warembo huwa wanawekwa sana karibu na waandaaji kuliko wengine na inatokea wao ndio washindi ! Na katika mashindano niliwahi kushiriki wanashinda watu ambao hutegemei na hawana vigezo kwa hiyo kwa mimi hili sioni ajabu sema limebainika tu Lakini mtindo wa uchakachuaji upo tu na utaendelea kuwepo... Kifupi Kamati ya miss Tanzania ni mbovu huwa haitendi haki na si wao tu kuanzia chini ...... Kwa mfano hapa juzi nilimsikia Wema redioni alisema aliombwa kushiriki na akaambiwa atakua miss Tanzania ... 

Sasa jiulize unapo ambiwa hivyo na warembo wengine wapo kwenye mashindano hapo inaleta picha gani ??? na ndio maana warembo hawajitokezi kwa sababu hakuna haki .... Binafsi mimi sio Sitti tu kuna warembo wengi ambao siwakubali na ninaowakubali ni wachache sana sidhani Kama wanazidi watano... Lakini wa kwanza miss Tanzania ninaemkubali kuliko wote ni Happiness(Millen) Magese wengine ni kufikiria"

No comments:

Post a Comment