Wednesday, October 15, 2014

Martin Kadinda Mmoja Wa Majaji Miss Tanzania 2014 Aupinga Ushindi Wa Sitti Mtemvu.

Sitti Mtemvu
Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu atakuwa amewaka historia kwa pengine kuwa mshindi wa Miss Tanzania aliyewahi kukataliwa zaidi na walio wengi kuwa hakustahili.
Mara baada tu ya Sitti Mtemvu kutangazwa mshindi weekend ilopita social media ukiwemo ukurasa wa Redds Tanzania ambao ndio wadhamini wakuu wa shindano hilo watu walitiririka muda mfupi kumkataa Sitti Mtemvu kuwa amependelewa hakuwa na vigezo huku Jihan Dimechk aliyesshika nafasi ya 3 wengi wakisema kuwa ndiye aliyestahili kuwa mshindi hivyo ameonelewa.

Martin Kadinda ambaye ni mdau mkubwa wa urembo na mitindo nchini alikuwa mmoja wa majaji wa shindano hilo katika kumtafuta Miss Talent. Martin ameweka wazi pia maoni yake kuwa Sitti hakustahili kuwa Miss Tanzania 2014, hakuwa na vigezo. Kadinda aliandika..........

"“Daaaaah… Anko Ludenga nakukubali Sana ila Kwa hili am not ur side!! sitti am not hating but Kwa upande wangu hapana.. I just wish u all the best Kwa majukumu yako And ukatuwakilishi vizuri maybe unaweza kufanya mazuri Zaidi Ya waliopita ila Kwangu wewe hapana…. Ukimind poa ila sio wote huwa tunakubaliana na matokeo…. Matusi noo Kwa my page.. Ukitukana nakublock"

                                                                   Kadinda


No comments:

Post a Comment