Monday, October 13, 2014

Lulu, Linah, Kemmy, Mama Kanumba Kutikisa Na Mapenzi Ya Mungu.

Hivi karibu Msanii Mahiri na Nguli katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kama LULU ataibuka na filamu yake Mpya na yenye kusisimua iitwayo "MAPENZI YA MUNGU" ambapo moja kati ya washiriki katika filamu hiyo ni Bi Flora Mtegoa ambae ni Mama Mzazi wa aliyekuwa Msanii Nguli wa Kiume Hapa nchini hayati Steven Kanumba.

Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni moja ya filamu ambayo Lulu ameonyesha uwezo wa hali ya na kuthibitisha kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike hapa Tanzania ambae ana kipaji cha hali ya juu katika kuuvaa uhusika ambapo ana uwezo wa kubadilika badilika kutokana na muongozo anaopewa. Ndani ya filamu hii pia yup Linah Sanga na msanii mkongwe wa filamu Kemmy Julieth Samson

Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa Sokoni hivi Karibu Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.

Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.


No comments:

Post a Comment