Friday, October 17, 2014

Kashfa Nzito Miss Tanzania ! Sitti Mtemvu Adaiwa Kuwa Na Mtoto, Majaji Hakuna Aliyejua Kifaransa, Wazazi Watofautiana Umri Wake.

Sitti Mtemvu
Kashfa imemwandama Miss Tanzania 2014, Sitti Mtevu baada ya vielelezo mbalimbali kuonyesha kuwa ameghushi umri.
Sitti katika fomu zake alijaza ana miaka 18, kitendo ambacho kimewashtua watu wengi na kuanza kufuatilia taarifa zake na kubaini kuwa passport yake inaonyesha ana miaka 25, huku mama yake mzazi akisema mwanae amezaliwa mwaka 1985 hivyo ana miaka 29, lakini cha kushangaza baba yake mzazi amesema Sitti ana miaka 18 huku kamati ya Miss Tanzania kupitia Bosco Majaliwa wakisema ana miaka 23
"umri wake ni kama alivyosema mwenyewe siku ile(miaka 18), kama mnataka kujiridhisha nendeni hata huko Miss Tanzania mtaoneshwa passport (hati ya kusafiria) yake....." amesema baba yake mzazi Sitti Mtemvu wakati akizungumza na Globalpublishers
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, mrembo huyo aliyetokea Kanda ya Temeke hakuwa na sifa za kushiriki mashindano kwa vile tayari alishavuka umri uliowekwa kikanuni na waandaaji wa shindano hilo.
Sifa za mshiriki wa Miss Tanzania, anatakiwa awe na umri wa miaka 18 hadi 23, awe raia wa Tanzania, awe hajaolewa, awe na ufahamu wa kutosha wa kujieleza, awe hajazaa, asiwe mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari.
Sitti
Pia, asiwe ameshiriki mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi yoyote zaidi ya mara moja kwa mwaka husika, maana yake hairuhusiwi kushiriki mara mbili katika mwaka mmoja. Lugha inayotumika ni Kiswahili na Kingereza.
Lakini, katika hali ya kushangaza, licha ya mrembo huyo kukiuka masharti hayo, alitangazwa kuwa Miss Tanzania mwaka huu, ushindi ambao umezua mjadala kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiponda ushindi wake na wengine wakienda mbali na kudai mrembo huyo ana mtoto mmoja huku baadhi ya watu wake wa karibu wakidaiwa kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa zake hizo.
Sitti
Vile vile habari nyingine zinasema kuwa majaji waliompam ushindi Sitti hawakuwa wakijua lugha ya kifaransa na watu wanaoijua lugha hiyo walisema kuwa licha ya Sitti kuchemka kujibu swali vizuri kwa kiingereza lakini pia alichapia kifaransa kwa mtu anayeijua lugha hiyo angebaini mapema.
                                               Sitti akiwa na baba yake mzazi

No comments:

Post a Comment