Tuesday, September 9, 2014

Nasomea Acting New York Film Academy Nataka Kuingia Hollywood: Winfrida Dominique Miss Universe Tanzania 2012.

Winfrida
Miss Universe Tanzania 2012 Winfrida Dominique ambaye pia ni 2013 Swahili Fashion Week Best Female Model Of The Year Kwasasa yupo nchini Marekani akisomea mambo ya uigizaji wa filamu katika chuo cha New York Film Academy.
Akizungumza exlusively na Swahiliworldplanet Winfrida mwenye vigezo vyote vya kuwa star mkubwa wa kimataifa alisema kuwa lengo lake ni kuwa muigizaji wa Hollywood ingawa pia bado anataka kuwa model wa kimataifa na hawezi kudharau filamu za nyumbani kwa madai sisi wenyewe ndiyo wa kuleta mabadiliko katika filamu zetu ziwe bora ambapo kwasasa bado zinachangamoto nyingi ikiwemo serikali kutosapoti sanaa.

"Nipo New York nasomea acting for film katika chuo cha New York film Academy huku nikiendelea na mambo ya mitindo kimataifa zaidi, nataka kuwa actress pia nasoma extensive training ya week nane, Dreams zangu ni Hollywood ila sitosita ku-share na film za nyumbani pia" Alisema mrembo huyo mwenye urefu wa kutosha na kupenda kuweka nywele zake kiasili.

Winfrida akiwa katika mafunzo ya ugizaji chuoni hapo
Winfrida wa pili kutoka kulia akiwa New York Film Academy.


Winfrida amesema pia kuwa anaendelea na kazi zake za mitindo kufanya akzi kimataifa zaidi pia. Angalia baadhi ya picha zake .....


Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment